Somo la 1

Kukadiria ni stadi muhimu katika Hisabati na sayansi. Mizani rahisi (zinazoweza kutengenezwa na zana za kufundishia rahisi sana) zinawawezesha wanafunzi kupima na kukadiria uzito kwa kutumia uchunguzi wa kimatendo.

Unaweza tengeneza mizani rahisi kwa kufanya shughuli hizi kwa kushirikiana na mwalimu wa sayansi katika shule yako. Hii itawafanya wanafunzi kuona jinsi masomo yanavyoingiliana.

Uchunguzi kifani ya 1: Kukadiria uzito

Bibi Bankole wa Uganda alikuwa akisoma uwalimu katika makao makuu ya wilaya yake. Kama sehemu ya somo la Hisabati kwa siku, mwezeshaji aliwasimulia hadithi hii. Halafu akawauliza walimu nini walifikiri mabinti hawa wanajua na wangefanya nini kama mabinti hawa wangalikuwa katika madarasa yao. ‘mabinti wawili, Nkechi na Lololi, walikuwa wanajadiliana juu ya uzito wa bisi zilizowekwa katika mifuko miwili, A na B, ambayo ilifanana kimaumbile na ukubwa. Nkechi alibeba mifuko hiyo na alistaajabu kuona B ulikuwa mzito zaidi kuliko A. alimwambia Lololi kuwa B ni nzito zaidi ya A. Lololi aliamua kuweka mifuko miwili katika sufuria mbili za mizani (angalia Nyenzo rejea 1 ). Aligundua kuwa katika mizani, mfuko B uliweza kushuka na hivyo basi B ni mzito zaidi kuliko A. Nkechi alipatia.’

Walimu walishughulika katika jozi, walitengeneza shughuli mbalimbali zilizomotisha kukadiria uzito, na baadaye kwa kutumia mizani walipima mawazo yao. Kila kundi lilifundisha madarasani kwao na baadaye kutoa taarifa katika kipindi kilichofuata. Bibi Bankole aligundua kuwa darasa lake lilipenda somo ila hakuwa na vitu vingi mbalimbali vya kutumia wanafunzi (kwa ushauri jinsi ya kuandaa zana, angalia Nyenzo rejea muhimu: Kuwa mwalimu mbunifu kuandaa somo katika mazingira magumu/ yenye changamoto ). Alisema safari ijayo atatumia muda mwingi kuandaa vitu vingi na ataunda makundi madogo madogo ya wanafunzi wanne hadi sita kuliko yale ya wanafunzi zaidi ya kumi.

Shughuli ya 1: Kulinganisha uzito

Unahitaji mizani rahisi tano (angalia Nyenzo rejea 1 ) na vitu vitano kama mawe, mipira, makopo, vizibo vya chupa, n.k. ambavyo unaweza kupima katika mizani rahisi ili kufanikisha zoezi hili. Hivi vitafutwe maeneo ya shule.

Andika maelezo yako kwa wanafunzi ubaoni. (angalia Nyenzo rejea 2: Maelezo kwa wanafunzi kwa ajili kukadiria na kulinganisha uzito ) na uwaelekeze wanafunzi nini unataka kufanya na vifaa hivyo.

Wape wanafunzi wawili vitu viwili na waambie wakadirie uzito

Sasa waambie wanafunzi kupima mawazo yao kwa kupima vitu katika mzani.

Waulize kipi ni kizito zaidi, na kwa nini wanafikiri hivyo. Waweke wanafunzi wako katika makundi matano, wape kila

kundi jozi ya vitu na mizani. Waambie wanafunzi kwanza

walinganishe uzito wa vitu hivyo. Waambie watumie mizani kutafuta na kulinganisha uzito wa vitu hivyo. (Angalia Nyenzo rejea Muhimu: Kutumia njia ya makundi darasani. )

Waambie wajaze jedwali la matokeo ili kuwaonyesha wengine darasani kuona kama watakubaliana nao.

Unaweza kuwapa changamoto wanafunzi wakubwa au wale wazuri kimasomo kuona kama ni kitu kipi kizito na kipi chepesi kabla ya kupima. Waweza tumia jedwali kama hili hapa chini. Je wanawezaje kuhakikisha matokeo yao kwa kutumia mizani?

ni mwepesi kuliko

Unyoya ---------------------- Chanio

Sehemu ya 4: Kupima uzito