Nyenzo-rejea ya 2: Maelezo kwa wanafunzi jinsi ya kukadiria na kulinganisha uzito
Nyenzo rejea ya mwalimu kwa ajili ya kupanga au kurekebisha ili kutumia na Wanafunzi
Aina C ya Nyenzo rejea: Nyenzo rejea mwalimu kwa ajili ya kupanga au kurekebisha ili kutumia na wanafunzi
1. Katika kundi, mmoja baada ya mwingine achukue vitu viwili na kuhisi uzito wake, mfano jiwe na punje ya maharage. Kipi kizito? Jaza jedwali hili hapa chini.
2. Mmojawapo katika kundi atumie mizani kulinganisha uzito na ajaze jedwali
3. Rudia hili kwa vifaa vyote, ukilinganisha vitu viwili kwa wakati mmoja, Ukiruhusu kila mmoja katika kundi kushiriki.
4. Weka jedwali mezani na kila mmoja kuangalia matokeo ya wenzake.
Kitu | Kipi kizito mikononi | Kipi kizito katika mizani |
---|---|---|
Mpira na punje ya maharage | mpira | mpira |
punje ya maharage na jiwe | jiwe | Jiwe |
Gunia la maharage na jiwe | ||
Nyenzo-rejea ya 1: Mizani rahisi