Somo la 1. Kupanga uchunguzi

Uchunguzi wowote unahitaji kupangwa na kufanywa kwa makini, vinginevyo matokeo yanaweza kuwa si sahihi au si ya uhakika. Katika Shughuli ya 1, utaangalia kauli inayohitaji kuonyeshwa kama ni sahihi au ni makosa. Hakikisha kwamba wanafunzi wako wamekamilisha mahitaji yao yote kabla hawajaanza uchunguzi, na kwamba wanaielewa kazi iliyoko mbele yao kabla hawajaanza kuifanya. Jukumu lako ni kuwasaidia wakati wanafanya kazi kwa kuuliza maswali ili kuchochea fikra zao na kuwahamasisha kuendeleza mawazo yao.

Uchunguzi Kifani cha 1: Kutumia maswala ili kujiandaa kwa ajili ya uchunguzi wa vitendo

Bibi Mwakapenda wa Afrika ya Kusini alitaka kuwapa wanafunzi wake uchunguzi wa vitendo kuhusu urefu ili kuona nani mrefu zaidi au mfupi zaidi darasani.

Aliwaandalia baadhi ya maswali ili kuhakikisha kwamba wameelewa kazi vizuri. Alianza somo lake kwa kujadili maswali na darasa zima (tazama Rejea ya 1: Sampuli ya maswali). Alikuwa anafahamu kwamba uchunguzi si tu kuhusu kupima. Ilikuwa pia kuhusu kukusanya na kurekodi data. Alitaka kuhakikisha kwamba wanafunzi wake walielewa nini hasa ingewahusisha.

Baada ya uchunguzi, Bibi Mwakapenda alifurahishwa sana na mafanikio ambayo wanafunzi wake waliyapata. Walionyesha kuwa walikuwa wanajua jinsi ya kuandaa uchunguzi. Walifanya uchunguzi sawa, na pia waliweza kupata vipimo sahihi vya umbali.

Shughuli 1: Nani anaweza kuruka mbali zaidi?

Anza kuwaambia wanafunzi wako kufikiria kauli ifuatayo na kujadili (katika makundi ya watu wanne) jinsi gani wangeweza kuchunguza kama ni kweli

'Mtu mrefu anaweza kuruka zaidi kuliko mtu mfupi.'

Kila kundi linahitaji upatikanaji wa kipimo cha tepu au rula au njia nyingine ya kupima kwa mfano mkanda au kamba. Jadili jinsi gani wanaweza kujibu swali na kukubaliana juu ya mchakato. Hii inaweza kuwa kama hivi:

  • chukua vipimo viwili kwa kila mtu na umpime kila mtu katika kikundi;
  • pima urefu kwa kusimama dhidi ya mizani kwenye ukuta ambayo uliitengeneza kabla ya kuanza somo;
  • urukaji lazima uwe wa 'kusimama' - mtu anasimama kwenye mstari, na kisha anaruka mbali jinsi anavyoweza;
  • pima urefu wa kuruka kwa kutumia tepu au mkanda n.k.

Waombe vikundi kujadili jinsi gani wanaweza kuonyesha matokeo (angalia Rejea 2:Njia mbili za kuangalia) Waulize kama vipimo vyao vinakubaliana na maelezo. Kama hapana, je wanaweza kuandika upya maelezo yao kulingana na matokeo yao?

Somo la 2. Kuruhusu wanafunzi kuandaa uchunguzi wao