Somo la 2. Kuruhusu wanafunzi kuandaa uchunguzi wao

Wakati wa kuchunguza mada kama vile kipimo, ni muhimu kutokimbilia kwenye dhana mpya bali kuwapa wanafunzi muda wa kuimarisha mafunzo yao na kufanya mazoezi katika ustadi mpya waliojifunza. Sehemu hii inatoa njia zaidi za kuchunguza ufahamu na uwezo wa wanafunzi kuweza kupima urefu katika mazingira tofauti.

Hapa, utawaomba wanafunzi wafanye mlinganisho baina ya vipimo na kufikiria uhusiano wowote uliopo. Kwa kutumia vikundi vilevile kwenye mfululizo wa shughuli, unaweza kugundua kama wanaweza kubaini na kuona uhusiano wa kufanana katika chunguzi mbalimbali kuweza kutumia data na mbinu walizotumia kabla.

Uchunguzi kifani 2: Maandalizi ya uchunguzi unaofanywa na mwanafunzi mwenyewe

Bibi Baguna aliamua kufanya kipimo kidogo cha upimaji pamoja na darasa lake ila kutoa mwongozo mdogo zaidi ukilinganisha na ule wa awali. Alitaka wawe huru zaidi na kutumia ujuzi waliojifunza kutokana na kazi iliyopita. Aliamua kusikiliza kwa makini wakati wakijadili jinsi ya kuendelea na kujua nani alikuwa anajitolea kufanya kazi. Alikuwa na shauku kujua nani aliweza kutambua kwamba wangeweza kutumia maarifa ya awali na njia za kufanyia kazi kwa kazi hii mpya.

Alifikiria kwa makini kazi gani abuni. Mwalimu mkuu alishazungumzia kuhusu suala la kusogeza uzio wa shule na lango la shule upande mmoja wa viwanja na kuupeleka mahala ambapo alisema ni karibu zaidi, ili kusaidia kuokoa fedha. Bibi Baguna hakuwa na uhakika kwamba ilikuwa ni karibu, na aliamua kwamba hili litakuwa ndilo tatizo halisi kwa darasa lake.

Alipanga tatizo hilo asubuhi na kuwaambia wanafunzi wake kwamba wangeweza kulifanyia kazi hadi mwisho wa siku. Iliwabidi pia kufanya kazi zao za lugha lakini alisema wangeweza kuchagua mpangilio wa kufanya kazi zao. Kwa vile alikuwa na tepu ndefu mbili tu za kupimia ambazo ziliazimwa kutoka ofisi za elimu, ilikuwa vigumu kuwa na idadi kubwa ya vikundi ambavyo vingeweza kufanya kazi kwa wakati mmoja. Wangeweza kutumia njia nyinginezo za kupima, kama vile kamba au mkanda. Alifurahishwa na jinsi walivyojipanga vizuri, na walipokuwa wanafanya kazi wenyewe, aliweza kuona nani aliyeweza kuelewa tatizo na jinsi ya kulitatua. Makundi yote yalikubaliana kwamba sehemu mpya kwa ajili ya njia ilikuwa ni karibu zaidi. Halafu aliwaambia wafanye hesabu kiasi gani cha fedha kinaweza kuokolewa kwa njia hiyo.

Walichukua uchunguzi wao kwa mwalimu mkuu ambaye alifurahishwa sana na habari.

Shughuli 2: Kuchunguza urefu dhidi ya usawa wa mkono

Anza kwa kuwaambia wanafunzi wako kwamba una uchunguzi mwingine ambao wao waufanye katika makundi yale yale ya awali.

Waulize ili kutambua kama kauli hii ni kweli:

'Urefu wako ni sawa na umbali kati ya vidole vyako na mikono yako inaponyooshwa.'

Waombe wajadili katika vikundi vyao:

  •  

    • Jinsi gani wangeweza kusahihisha maelezo haya?
    • Watapima nini?
    • Vitengo gani vya vipimo itabidi watumie?
    • Vipi wataandaa kazi?
    • Vipi watarekodi matokeo yao?

Baadaye, waombe wafanye uchunguzi kwa pamoja, au katika nyakati tofauti (kutegemea uwezo wako), na nenda karibu nao ukiwasikiliza huku wakifanya kazi, ukiwasaidia kama wana tatizo. Waombe wakuonyeshe jinsi gani waliweza kupata jibu. Yaonyeshe majibu yao.

Jadiliana nao nini umeona jinsi wanavyofanya kazi kwa vikundi.

Vipi unaweza kuwasaidia kufanya kazi bora kwa vikundi? (Angalia Rejea Muhimu: Kutumia njia ya kufanya kazi kwa vikundi darasani)

Somo la 1. Kupanga uchunguzi

Somo la 3. Kutathmini ufahamu wa urefu