Somo la 3. Kutathmini ufahamu wa urefu

Ni muhimu wanafunzi waelewe 'kihalisi' tofauti ya vipimo vya urefu mbalimbali na kuweza kukadiria na kupima urefu wa kitu kwa kusimama na kwa kulala. Huu ni ujuzi muhimu sana katika maisha halisi. Kwa mfano, je mti utaangukia nyumba yetu au utaangukia chini kama uking'olewa? Kutathmini kama wana hii hisia 'kihalisi', unaweza kutumia swali kutatua katika karatasi ambapo watahitajika kutumia akili zao, au kuwapa uchunguzi wa mwisho kuhusu kitu halisi, kama vile katika Shughuli Muhimu.

Kazi ikimalizika, wahimize wanafunzi wako kujua zaidi kuhusu miti ya asili ya nchi yako na jaribu kupima mti mkubwa karibu na shule yako kama mti upo. Kufanya kazi kwa njia hii ya vitendo kutajenga imani yao katika kukabiliana na urefu.

Uchunguzi kifani 3: Kutathmini ufahamu wa urefu

Bibi Juma kutoka Tororo Rock alitaka kujua kama wanafunzi wake walikuwa na uelewa halisi wa aina tofauti za urefu, hivyo aliunda kitendo katika karatasi ambapo iliwabidi wanafunzi wafanye binafsi ili kuchunguza suala hili. Alinakili kitendo kwenye ubao (tazama Rejea 3:Swali juu ya urefu) Aliwaambia wanafunzi wake, waliopo Msingi darasa la 6, kufanya kazi binafsi na kufikiria kwa makini kuhusu majibu kabla ya kujaza nafasi zilizo wazi. Alikusanya vitabu vyao na kuangalia majibu yao.

Bibi Juma alitambua kwamba wengi wa wanafunzi wake walikuwa bado hawajapata hisia ya uhalisi kuhusu urefu na hivyo aliamua kufanya vitendo zaidi. Aliwaambia kupima maeneo ya shule lakini ilibidi kwanza kukadiria urefu wa kila upande na kuurekodi. Kila kikundi kilichukua zamu kupima kwa vile yeye alikuwa na tepu moja tu ndefu kwa ajili ya kupimia. Alitengeneza orodha kubwa ya vipimo muhimu na kila kikundi kiliweka vipimo vyao wenyewe kila walipomaliza. Hakuwaonyesha hiyo orodha hadi hapo makundi yote yalipomaliza, hivyo wasingeweza kuathiriwa na matokeo ya wenzao. (Alipanga kutumia data hii baadaye kwa somo la SST ili kutenegeneza ramani ndogo ya eneo la shule.)

Wakati wanafunzi wote walipomaliza kupima, alijadili pamoja nao tofauti katika vipimo vyao na kisha aliwauliza kwa nini ilikuwa hivyo. Waliweza kupendekeza baadhi ya sababu nzuri kama vile kuanzia katika maeneo tofauti, na pia kutoweka kipimo cha tepu ya kupimia sawasawa.

Shughuli muhimu: Mti mkubwa una ukubwa gani?

Soma dondoo ifuatayo kuhusu 'Mti Mkubwa' darasani.

Soma Rejea 4: Mti mkubwa katika msitu wa Budongo kabla ya kupanga somo, bora fikiria jinsi utakavyoweza kurekibisha hii kwa mahitaji ya wanafunzi wako. Utahitaji kupata tepu ndefu sana ya kupimia.

Kama inawezekana, chukua wanafunzi wako nje pale ambapo kuna nafasi nyingi; vinginevyo, tumia ukumbi mkubwa ili kujaribu vitendo. Utahitaji kiasi cha wanafunzi 60 wenye wastani wa urefu wa m 1 kwa urefu na hivyo unaweza kuamua kuchanganya na darasa lingine. Fanya kazi na darasa zima kwa pamoja na waulize maswali elekezi ili kuwasaidia kutatua tatizo.

  • 'Katika msitu wa Budongo kuna miti mikubwa mizee ya mikangazi. Baadhi yao ni m 60 kwenda juu na huwa na mduara wa m 6 au zaidi.'

Waonyeshe picha wakati unanza somo lako na kisha fanya vitendo katika Rejea 4.

Ukimaliza nje, walete wanafunzi wako ndani na waambie wajibu maswali katika Rejea 4 ili kupima uelewa wao.

Somo lijalo, waambiye wafanye maonyesho ya shughuli zao zote za kupima na waalike madarasa mengine kuja kuona kazi zao.

Somo la 2. Kuruhusu wanafunzi kuandaa uchunguzi wao