Mti mkubwa katika msitu wa Budongo

Nyenzo za mwalimu kwa madhumuni ya kupanga au kurekibisha kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi

Urefu wa mti kubwa

Wakumbushe wanafunzi wako kuwa urefu wa mti ni mita 60. Waulize:

‘Je unafikiri pindi kama wanafunzi wote hapa wangepangana mmoja juu ya mwenzake kwa vichwa kuelekea juu, unafikiri hatimaye wangefika juu ya kilele cha mti huu?

Hilo halingekuwa rahisi na hivyo tunaweza kufanya nini? Ndiyo, tungejaribu kulala chini badili yake.

Hebu tufanye hivyo.’

Waombe wanafunzi kumi walale chini na mwambie mwanafunzi mwingine apime na kuona kama inatosha.

Sasa uliza: Itachukuwa wanafunzi wangapi unafikiri?

Ongeza wanafunzi zaidi hadi ujue itafikia wangapi kutimiza m 60.

Hatimaye, muulize mmoja wao kuelezea jinsi gani urefu wa mti mkubwa ulivyo.

Mzingo wa mti mkubwa

Tunaambiwa kwamba Mzingo wa mti ni mita 6. Waulize wanafunzi wako:

'Mnafikiri itachukua wanafunzi wangapi kama wakitaka kufanya pete kuzunguka mti, na vidole vikiwa vinagusana?'

Jaribu kwa kumwambia mwanafunzi mmoja kupima m 6. Kisha unda duara na wahesabu wanafunzi – hii itakupa wazo la Mzingo wa mti.

Sasa jaribu maswali haya na kikundi chako:

  1. Kabla ya shughuli hii nilidhani m 60:
    • a.Ni urefu kama jengo la shule
    • b.Ni urefu kama mlima
    • c.Ni urefu kama mti mrefu
    • d.Ni urefu kama mnara wa simu
    • e.Sikufikiria kuhusu hilo
  2. Itachukua idadi ya wanafunzi ifuatayo ili kufanya pete kuzunguka mti mkubwa katika msitu wa Budongo:
    • a.Angalau 7
    • b.Angalau 6
    • c.Angalau 5
    • d.Angalau 4
    • e.Angalau 3
  3. Mita 1 kwa urefu ni takriban:
    • a.Umbali kutoka ncha ya pua ya mtu wa wastani hadi vidoleni mwake wakati mikono imenyoshwa
    • b.Urefu wa mtu wastani
    • c.Urefu wa meza ndogo
    • d.Urefu wa ng'ombe