Sehemu ya 3: Kuangalia vimiminika

Swali Lengwa muhimu: Ni jinsi gani utatumia njia mbalimbali kuchunguza vimiminika?

Maneno muhimu: Upimaji; ramani ya mawazo; maelezo; mvuto wa uso; uchunguzi;

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • umetumia picha kubwa ‘ramani ya mawazo’ katika kuona ni nini ambacho tayari wanafunzi wanakijua wakati unaanza mada mpya;
  • kufanya maonyesho ya vitendo darasani kutoa changamoto ya fikra kwa wanafunzi;
  • Kupanga aina mbalimbali za shughuli ikiwa ni pamoja na uchunguzi na maigizo ili kujenga uelewa wa wanafunzi juu ya kazi/dhima za maji.

Utangulizi

Haijalishi ni umri gani unaoshughulika nao, ni vizuri zaidi kuanza mada kwa kuwafikirisha wanafunzi ambapo utaweza kutambua vitu ambavyo tayari wanavijua. Hii inaweza kuandikwa katika umbo kama ramani ya mawazo (angalia Nyenzo rejea muhimu: kutumia ramani mawazo na majadiliano kugundua mawazo ). Wahamasishe wanafunzi kuchangia maswali yoyote na mawazo waliyo nayo. Kujua mahitaji ya wanafunzi wako katika kujifunza kutakusaidia zaidi kuandaa kwa njia sahihi. Ni vitu gani lazima vipangwe? ( Nyenzo rejea Muhimu: kupanga na kuandaa masomo yako)

Katika sehemu hii tunakuongoza juu ya kutumia ramani ya mawazo na kuandaa shughuli mbalimbali kuhusu vimiminika na tabia zake.

Nyenzo ya 5: Molekyuli na Atomu