Somo la 1

Unajuaje,(mwalimu) wanachokijua wanafunzi kuhusu nguvu na mwendo? Na unawezaje kupanua mawazo haya na kuhusianisha na ufahamu wa kisayansi ya kisasa?

Katika uchunguzi kifani 1, mwalimu anaongeza ufahamu wa matukio yote ya nguvu yanayowazunguka. Kutoka mwanzo, anawapa changamoto juu ya uelewa wao kwa kuwaomba kujiona wenyewe kama watafiti wenye upeo wa kisayansi

Katika shughuli 1, unawaomba wanafunzi kuchunguza na kuelezea nguvu zinazojitokeza kwenye picha. Kwa kujaribu kupambanua kile walichochunguza , watakuwa wanaongeza ufahamu wa kisayansi kwa msaada wako.

Uchunguzi kifani ya 1: Kuwapa changamoto wanafunzi kuona nguvu kila mahali

Eugenia akiwa Abuja, Nigeria ni mwalimu mwenye uzoefu aliyejifunza kuwaamini wanafunzi wake. Alipokuwa akisoma miaka michache iliyopita, alitambua namna ufundishaji wakizamani unao mweka mwalimu kama ndio chanzo pekee cha maarifa na mwanafunzi kama mpokeaji tu wa maarifa ulivyomfanya mwalimu kupuuza mchango wa wanafunzi. Sasa anafundisha kidogo na kuwapa changamoto nyingi.

Alianza mada ya ‘nguvu’ kwa kupendekeza wanafunzi kuwa wana ‘JUMA LA NGUVU’, ambapo karibu kila kitu kinachotokea kitahitaji maelezo kuhusiana na mawazo juu ya nguvu na mwendo. Kitu cha kwanza jumatatu, walivyo andika tarehe kwenye daftari zao, aliwaambia waache

na kufikiri kama kuna nguvu yoyote imetumika katika kuandika. Majadiliano motomoto yalifuata. Aliwahamasisha kuchunguza kwa kuweka alama mbalimbali kwenye makaratasi. Walikuja na mawazo ambayo yalimshangaza na hata kumpa changamoto. Tunavuta kalamu kukatiza karatasi;

‘Lakini mimi nasukuma kalamu’ Danladi anayetumia mkono wa kushoto alishangaa

Peni huteleza kiurahisi zaidi kuliko kalamu ya risasi’- Labda wino ni kama mafuta kwenye baiskeli

‘Angalia, unasukuma na unavuta wakati unasugua. Kusugua ni nguvu nyingine tofauti. Unafunguaje ukurasa mwingine unaposoma kitabu? Swali hili lilileta mjadala zaidi juu ya msukumo wa taratibu, mivuto na unyanyuaji na kushikilia kitabu dhidi ya uzito.Kutambua nguvu zinazotokea kila siku hakika iliwashangaza wanafunzi. Mara, wakajadili na kujaribu kuelezea matukio mengi ya aina hiyo.

Shughuli ya 1: Uchunguzi wa nguvu katika picha

Unahitajika kukusanya picha nzuri kutoka magazetini au machapisho yanayoonesha nguvu katika vitendo na athari zake. Waombe baadhi ya wanafunzi kukusaidia kukata mishale yenye rangi mbili kwenye karatasi (imewekwa rangi kwa kuvuta na kusukuma) na saizi tatu. (Nyenzo rejea 1: kuchunguza nguvu kwenye picha.)

Wanafunzi watatu watatu wafanye kazi kuangalia kwa makini picha kuona nguvu katika vitendo. Weka alama mivuto na misukumo yote inayoonesha uelekeo wa nguvu na jiandae kujadili na kushirikishana kwa kile wanachoamini. Angalia kama wanatambua kuwa mishale ya saizi tofauti inaweza kutumika kulinganisha nguvu tofauti wanazoona. Je wanagundua kuwa unapata mabadiliko katika mwendo wakati nguvu haziposawa?

Wanafunzi wakae katika makundi ya watu sita sita kuelezea, kuchunguza na kupeana changamoto katika mawazo yao.

Kuwakusanya watu sita sita kutathmini kazi zao kutakuwa na mafanikio? Je, ilisaidia kila kundi kuelewa ukubwa, uelekeo na athari za nguvu vizuri?

Sehemu ya 1: Nguvu za kila siku-uchunguzi wa mwendo