Somo la 2

Nguvu na mwendo ni sehemu ya michezo na burudani kwa watoto. Unaweza kutumia hii kupima wanachokifahamu wanafunzi na kuwasaidia wao katika kuchanganua fikira zao wenyewe. Kwa kufanya hivi, watakuwa wanapanua uelewa wao.

Uchunguzi kifani 2 unaonyesha jinsi wanafunzi wanavyoweza kujifunza kuhusu nguvu na mwendo kupitia michezo na mashindano.

Shughuli 2 inajengwa kwenye utambuzi wa wanafunzi wa nguvu/kani kutoka shughuli 1. Tunawianisha kazi za sayansi na lugha kutusaidia kuelezea nguvu na athari zake kwa uhakika katika chemshabongo. (rejea Nyenzo muhimu: Matumizi ya ramani ya kumbukumbu na chemshabongo kuibua mawazo.) Hakuna majibu sahihi na yasiyo sahihi katika chemshabongo, lakini unawapa changamoto wanafunzi kufikiri kwa kuwahamasisha kutoa mawazo yao. Sehemu muhimu ya kujifunza katika sayansi ni kubadilishana mawazo na kwa kutumia lugha ya kisayansi

Uchunguzi kifani ya 2: Mashindano ya Olimpiki

Julius Maganga aliandaa michezo na mashindano siku ya Ijumaa. Alitafakari kwa makini namna michezo itakavyoonyesha dhana ya nguvu. Alitambua kwamba kuvutana kikono kungeonyesha namna nguvu inavyofanya kazi katika jozi ya watu na kwamba, kama pande zote mbili zina nguvu sawa, kutakuwa hakuna mwendo. Alifikiri jinsi ya kutumia mpira kuonyesha nguvu inayofanya kazi kwenye kitu kilicho katika mwendo-upepo unaovuma kwenye majani makavu unaweza kusababisha mwendo, badiliko la mwelekeo na kupunguza au hata kusimamisha mpira wa mezani. Mvutano ungeweza kuwafanya wanafunzi wafikiri kuhusu ulingano na kutokuwa na ulingano.

Kabla ya kila mchezo, Maganga aliwauliza wanafunzi kutabiri mchezo gani utawafundisha kuhusu nguvu. Halafu, mchezo ukiwa unaendelea, alichukua jukumu la utangazaji, kuelezea kilichokuwa kinatokea na kutoa taarifa za ziada kuhusu athari za nguvu. Kwa njia hii walikuwa wakifikiri kuhusu nguvu iliyotumika kadili walivyoona athari zake moja kwa moja. 

Juma lililofuata, Maganga na wanafunzi walijikumbusha juu ya ‘nguvu za Olimpiki’ na walitengeneza nakala na michoro kuonyesha walichojifunza. (Angalia Nyenzo rejea 2: Michezo ya Nguvu.)

Shughuli ya 2: Maneno yanayoonyesha nguvu ndani yake(vitendo)

Andika kwa nafasi maneno haya ubaoni (au kwenye karatasi tofauti)’ sukuma’, vuta’, na chezesha/geuza’.

Wanafunzi wafikirie maneno yote yanayoashiria nguvu na kuonyesha jinsi kila neno linavyotamkwa. (Angalia Nyenzo rejea 3 : Utamkaji wa maneno yanayoonyesha nguvu kutoka mifano ya wanafunzi .) Wahamasishe wanafunzi kutumia lugha zote wanazozijua na kuzitumia. Kuna maneno yanayotamkwa/sikika kama tendo lake lilivyo? Fikiri maneno kama ‘choma’ au ‘dunda’, na hata ‘vuta’, au ‘paka’ (tia doa).

Jadili maneno na vitendo pamoja na wanafunzi, kwa kuigiza. (mfano, unafanya nini unapokamua kitambaa kutoa maji?). Angalia kama maneno yanaonyesha msukumo, mvuto au mwendo mzunguko. Tegemea baadhi kutokukubali kabisa. Wape wanafunzi muda kujadili mgongano wa mawazo na kutambua mchango wenye mantiki.

Mwisho, waandae wanafunzi kuonesha maneno yaliyochaguliwa pamoja na picha zake au vitu vinavyoonyesha matendo ya nguvu (mfano, nati inaweza kuonesha tendo la kufunga nati, ‘bisibisi’ ‘rarua’ inaweza kuonesha kitambaa kitichotoboka.