Nyenzo rejea 6: Dhana nyingine kwa majaribio ya nguvu

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Kutumia springi kupimia nguvu:

Tengeneza orodha ya kila kitu walichokiona wanafunzi ukijumuisha springi

Onyesha jinsi springi zinavyonyumbuka kukiwa na nguvu inayovuta na pima kiasi gani inanyumbuka.

Tumia springi kupima nguvu darasani-pima jinsi springi zinavyobadilika katika urefu. (unaweza kutengeneza springi kutoka urefu wa sm 50 za waya wa shaba nyekundu au unaweza kutumia utepe imara unaotanuka badala ya springi.) nguvu nyingine za kupima zinajumuisha kufungua mlango, kuvuta kiti sakafuni, kuvuta peni au kalamu, kufungua kibanio cha nguo. kupunguza msuguano majini-kutengeneza maumbo yaliyonyoka:

Waombe wanafunzi kuchora maumbo mbalimbali ya samaki, mitumbwi na ndege. Ni umbo lipi zuri kwa kwenda kwa kasi hewani au majini?

Wanafunzi watengeneze maumbo mbalimbali kwa kutumia udongo. Dondosha maumbo hayo kwenye tanki refu la maji na angalia muda gani yanachukua kufika chini ya tanki.

Nguvu kwenye umbali fulani:

Tumia sumaku kuchukua pini za chuma. Waeleze wanafunzi kusogeza sumaku taratibu kuelekea kwenye pini. Kuna umbali gani kati ya sumaku na pini wakati pini inapoanza kuondoka?

Sugua bomba la peni (la plastiki) au rula kwenye nguo(mfano kifutio). Hii hufanya peni au rula ziwe na kiasi fulani cha umeme. Sasa jaribu kutumia peni au rula kuchukua kipande kidogo cha karatasi. Itavichukua vingapi?

Watake wanafunzi kuelezea kinachotokea katika kila jaribio. Nguvu na uzito:

Uzito ni nguvu za aina yake zilizosababishwa na dunia kuvuta kila kitu juu yake au karibu nayo.

Waombe wanafunzi kutumia springi au utepe mnyumbuko kutengeneza mizani inayopima mvuto wa dunia katika vitu. Watahitajika kutengeneza kipimo (skeli)

Halafu ongea na wanafunzi namna uzito wa vitu hivi unavyoweza kuwa tofauti kwenye sayari nyingine katika mfumo wa jua au katika mwezi. Sayari kubwa zina nguvu mvutano kubwa katika kitu fulani na sayari ndogo zina nguvu ndogo.

Nyenzo-rejea 5: Tunawezaje kupunguza msuguano?

Sehemu ya 2: Uchunguzi wa sauti na muziki