Sehemu ya 2: Uchunguzi wa sauti na muziki

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kuwahusisha wanafunzi katika tathmini?

Maneno muhimu: sauti; zana za muziki; tathmini; rasilimali za mahali; mchezo, mradi

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Umetumia tathmini ya wanafunzi wa rika moja ;
  • Umetumia rasilimali kutoka jamii husika katika kutengeneza zana za muziki pamoja na wanafunzi wako;
  • Umetumia shughuli za vitendo kupanua uelewa wa wanafunzi wako juu ya namna ya kubuni sauti mbalimbali.

Utangulizi

Kutoka utotoni, tunaitikia kwa sauti zinazozoelekea-mtoto ataitikia sauti ya mama au mlezi wake kwa mfano-na tunajifunza sauti mpya haraka sana. Wanafunzi wako watakuwa wamejifunza kutambua sauti mbalimbali. Katika sehemu hii, uwasaidie kupanua mawazo ya wanafunzi wako kuhusu sauti na namna zinavyotolewa. Msisitizo ni shughuli za vitendo na kujifunza kwa juhudi. Unaweza kupiga zana mwenyewe? Au unajua mtu ambaye anaweza kutembelea darasa kuwapigia zana wanafunzi wako?

Sehemu hii pia inatafiti njia za kusaidia wanafunzi kutathmini kazi zao.( Angalia Nyenzo muhimu: Tathmini ya mafunzo.) kuhusishwa katika tathmini husaidia wanafunzi kuelewa mafunzo na kupanga malengo ya baadaye. Pia hujenga kujiamini na hamu ya kujifunza.

Nyenzo rejea 6: Dhana nyingine kwa majaribio ya nguvu