Somo la 1

Mara nyingi ni vizuri kuanza kwa kufahamu kile wanachokijua wanafunzi. Wanafunzi watatambua sauti nyingi tofauti tofauti, lakini inawezekana hawajazingatia utofauti wa sauti hizi kama sauti ya juu au ya chini na uzito wa sauti (sauti nzito au nyororo).

Katika Shughuli 1, unafanya mchezo wa kukisia pamoja na wanafunzi wako, ambapo wanatambua sauti na kuelezea namna wanavyofikiri jinsi sauti zilivyotengenezwa. Hii inahusisha wanafunzi kuhesabu majibu wanayopata, njia mojawapo ya kuwahusisha katika tathmini.

Usitupe majibu yanayoonekana kuwa si sahihi-wahamasishe wanafunzi kuelezea sababu zao. Unaweza kujifunza mengi kuhusiana na uelewa wao kutokana na kile wanachosema. Baadae, fikiria kuhusu

walichokisema-kulikuwa na chochote kilichokushangaza?

Uchunguzi kifani 1 unaonesha namna mwalimu mmoja alivyotumia hadithi ya mahali kama sehemu ya wanafunzi kuuliza kuhuisu sauti. Je, unaijua hadithi yeyote kutoka katika utamaduni wako unayoweza kuitumia? Au unaweza kumwalika mwanajamii mmoja kutembelea shuleni kuhadithia hadithi? Mmoja wapo wa wanafunzi anaweza kuhadithia hadithi?

Uchunguzi kifani ya 1: Kutumia hadithi za jamii(hekaya) kuanzisha mada ‘sauti’

Bi. Sarpong, ambaye anafundisha huko Afrika ya Kusini lakini ametokea

Nigeria, alitumia hadithi za Kinigeria kuhusu ngoma kuanzisha mada

’sauti’ (Angalia Nyenzo rejea1: hadithi za sauti)

Alipowasimulia hadithi wanafunzi, alipiga aina tatu tofauti za ngoma ili kuonyesha midundo ya sauti za ngoma katika hadithi.

Baada ya kusimulia hadithi, walijadili kuhusu sauti katika hadithi na namna zilivyotengenezwa.

Baadhi ya makundi yalichunguza jinsi ngoma zinavyotoa sauti kwa kutumia mchele ju ya ngoma na kuona mtikisiko wake. Pia walijaribu kupata sauti tofauti kutoka ngoma ileile.

Makundi mengine yalichunguza kinachotokea wakati walipopitisha hewa juu ya midomo ya chupa tupu za plastiki. Waliweka dondoo ya kile walichokiona na baadaye, walishirikishana walichofikiri kabla na walichojifunza.

Mwishowe, walitengeneza orodha ya maswali yote waliyokuwa nayo kuhusu sauti na kubandika ukutani. Saprong aliwahamasisha kufikiria njia wanazoweza kupata majibu wao wenyewe.

Shughuli ya 1: Mchezo wa kubuni sauti

Kusanya vitu tofauti 10-12 vinavyotoa sauti za kuvutia-jumuisha sauti zinazofahamika na zisizofahamika. Unaweza kujumuisha sauti zilizonakiliwa kwenye simu za mkononi. Kabla ya wanafunzi hawajafika darasani, utahitajika kuficha luninga lusioneshe vitu na vitendo vinavyotoa sauti.

Watulize wanafunzi na uwaelezee ulichopanga. Waambie kwamba watatakiwa kutathmini sauti kiuungwana.

Nyuma ya luninga, weka sauti fulani kwa zamu. Wanafunzi wanatakiwa kuandika namna wanavyofikiri sauti zinatengenezwa.

Mwishoni, onyesha jinsi kila sauti ilivyotengenezwa na wanafunzi wahesabu sauti walizotambua

Mwishowe, waulize wanafunzi kama sauti zote zilikuwa rahisi kuzitambua? Namna gani waliweza kutambua sauti wasizozizoea? Dondoo gani ziliwasaidia kutambua hizo sauti?

Sehemu ya 2: Uchunguzi wa sauti na muziki