Somo la 2

Sauti zinatengenezwa kwa vitu vinavyotetema. Kitu kinachotetema kinasababisha chembechembe za hewa kusafiri pamoja na halafu zinaachana kwa mfumo fulani-hii huitwa mawimbi ya sauti (angalia Nyenzo rejea 2: Mawimbi ya sauti). Hivyo hewa hupeleka sauti kwenye masikio yetu.

Katika shughili 2 watake wanafunzi kutumia vitu vya kila siku kutengenezea sauti na kuona namna wanavyoweza kubadili sauti kwa njia tofauti tofauti. Wanafunzi lazima wafanye utafiti huu katika makundi madogo (rejea Nyenzo Muhimu: Matumizi ya kazi za kundi darasani). Tumia muda fulani mwishoni mwa utafiti kuzungumza na wanafunzi kuhusu namna makundi yalivyofanya kazi; je wana mawazo kuhusu jinsi ya kufanya kazi pamoja kwa ufanisi zaidi wakati ujao?

Katika uchunguzi kifani 2 , mwalimu anatumia jozi ya maswali yanayovuta hamasa kuwasaidia wanafunzi kufikiri kuhusu kazi zao-njia nyingine ya kuwahusisha kwenye tathmini.

Uchunguzi kifani ya 2: Upimaji wa umbali wa kusafiri kwa sauti

Abdalla alipanga wanafunzi mchanganyiko, wanaotofautiana kiumri katika makundi sita. Kila kundi lilipewa baadhi ya vipande vya mbao.

Aliwaambia kutafiti umbali wa sauti za vipande vya mbao vilivyobamizwa pamoja. Kila kundi lilifanya uchunguzi wake. (rejea nyenzo muhimu; matumizi ya tafiti darasani). Walipoandaa utafiti wao na kuamua atakaye shughulika na kila zoezi, aliwataka wafanyie kazi nje. Makundi yalirekodi matokeo kwenye bango.

Baada ya kumaliza tafiti zao, Abdallah aliwapa maswali yafuatayo kujadili kwenye makundi yao:

Walipata jibu sahihi la swali (matokeo)? Waliridhishwa na kumbukumbu zao? Wangefanya nini tofauti safari nyingine?

Abdallah alijua hii ni njia nzuri kuwasaidia wanafunzi wake kufikiri juu ya mafunzo yao. Wanafunzi walikuja na baadhi ya mawazo mazuri sana kujumuisha kuwa upepo ulitofautiana na kuathiri matokeo, siyo kusikia kwa kila mmoja kunafanana na kwamba kelele nyingine zilikuwa zinazuia.

Shughuli ya 2: Utafiti wa mabadiliko ya sauti.

Panga wanafunzi katika makundi madogo ili kutafiti njia za kubadili sauti zilizotengenezwa na vitu mbalimbali. Wape kila kundi jozi moja ya vifaa- haya ni baadhi ya mawazo:

Tumia madebe ya ukubwa tofauti kama ngoma

Jaza maji bilauri tano zinazofanana katika viwango vinavyotofautiana na weka alama kwa kalamu ya risasi.

Pitisha hewa juu ya chupa nne za ukubwa tofauti tofauti

Tumia chupa nne za plastiki zinazofanana na zilizojaa kiasi tofauti cha mchanga

Wanafunzi wanaweza kuchagua kitu chochote:

Watake wanafunzi kufikiri na halafu kufanya uchunguzi: Unatengenezaje sauti?

Unawezaje kufanya sauti iwe ya juu? Chini? Yakusikika?

Kila kundi linarekodi matokeo yao kwenye bango, ikijumuisha mfumo wowote waliougundua. Pia wanajadili:

kwa kiwango gani wamefanya kazi pamoja; namna wanavyoweza kujipanga muda mwingine; Namna walivyofurahishwa na michango ya kundi juu ya mabadiliko ya sauti.

Makundi yanaweza kubadili vifaa kama wanapenda kufanya uchunguzi mwingine, lakini hakikisha wamekwisha kurekodi matokea yao katika bango au katika daftari.

Unaweza kutumia Nyenzo rejea 3: mawazo wanayoweza kuwa nayo wanafunzi kuhusu kufanya kazi kimakundi kusaidia wanafunzi wako katika majadiliano yao mwishoni mwa jaribio.