Sehemu ya 3: Kuchunguza umeme

Swali Lengwa muhimu: Unaweza kufanya shughuli gani za umeme kwa vitendo darasani kwako?

Maneno muhimu: umeme; saketi: sumaku umeme; mifano; uchunguzi; kazi ya kikundi

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Umepata ujasiri wa kufanya shughuli za umeme kwa vitendo darasani kwako na kuelewa zaidi juu ya hatari zinazohusiana na umeme;
  • Umetumia kazi za vikundi kwa mzunguko;
  • Umewasaidia wanafunzi wako kufanya uchunguzi wakiwa kwenye makundi madogo.

Utangulizi

Sehemu hii inahusika na umeme. Mada hii mara nyingi huwaogopesha waalimu-unaweza kudhani kuwa ina mambo mengi, ngumu au hata ni hatari. Lakini kuna shughuli za vitendo ambazo moja kwa moja zinamsaidia mwanafunzi ajenge maana ya eneo muhimu la maisha ya kisasa.

Tunashauri utumie makundi madogo kufafanua na kuchunguza ili kuwasaidia wanafunzi waelewe mawazo mawili ya msingi:

Nishati haiwezi kutengenezwa au kuharibiwa, bali inaweza kubadilishwa kutoka hali moja hadi nyingine. Tunaweza kubadili nishati ya umeme kuwa nini?

Kifaa cha umeme kitafanya kazi pale tu ambapo kutakuwa na mzunguko kamili ya mkondo wa umeme

Nyenzo-rejea 5: Zana asili za muziki