Nyenzo-rejea ya 1: Kuangalia balbu ya tochi kwa makini

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Kwanza tengeneza zana zako za kufundishia- mfano wa balbu ya tochi, na soma habari hii juu ya balbu ya tochi.

Kwa wanafunzi wadogo, tunashauri utumie sehemu ya uso kuelezea nini tunamaanisha tunaposema sehemu za kitu.

Sasa liambie darasa kuwa litafanya vivyo hivyo kwenye balbu ya tochi. Lipange darasa lako katika makundi ya watu watatu/wanne:

Wape kila kundi balbu ya tochi na waambie waingalie kwa makini. Nini sehemu za balbu?

Wape dakika chache kuziangalia kwa makini.

Wakati wakifanya hivi, chora mfano wa balbu ya tochi ubaoni (au unaweza kuwa na mchoro uliochorwa tayari, ambao utauonyesha wakati huu. Pia unaweza kuwa na violezo, vilivyoandikwa kwenye kadi, tayari kuonyesha pale watakapokwambia nini wamekiona.)

Wanapoonekana kuwa tayari, waambie wakwambie walichokiona. Unaweza kuwa wazi kwa ushauri wowote na jaza ushauri huo pichani kwa mpangilio usio rasmi. Au unawezakuamua kutumia mpangilio rasmi na kuongoza mtazamo wao kwa kuonyesha sehemu kwenye mchoro na kuuliza maswali maalum. Jinsi wanavyojibu, chora na elezea sehemu- muhutasari ufuatao utakuonyesha jinsi ya kufanya.

Kuandika uchunguzi katika mpangilio mzuri

Elekeza kwenye sehemu ya duara ya balbu. Tunaona nini hapa?

Jibu: Kioo cha mviringo

Ndani ya huu mviringo wa kioo tunaona nini?

Jibu: Nyaya mbili nene

Tunaona nini kati ya nyaya mbili nene?

Jibu: Waya mwembamba, kama nywele iliyojikunja, unaoitwa filamenti.

Tunaona nini kati ya nyaya mbili nene karibu na shina/kwa chini?

Jibu: Shanga ndogo ya kioo

Nini kiko chini ya balbu ya kioo?

Jibu: Ngoma ya metali/kasha/silinda

Tunaweza kuangalia nini kwenye upande moja wa kasha lametali, karibu na sehemu ya juu?

Jibu: Taa ndogo ya metali

Tunaona nini chini ya balbu ya tochi?

Jibu: Metali/ncha ya risasi

Tunaona nini kati ya kasha la metali na ncha ya metali/risasi?

Jibu: Plastiki nyeusi

Kuna kitu kingine chochote ulichoona?

Jibu: Wengine wanaweza kuona

maandishi kwenye kasha la metali.

Kutengeneza zana ya kufundishia

Pia unatakiwa utengeneze mfano wa balbu ya tochi kubwa kwa ajili ya shughuli ambapo wanafunzi wanaona balbu kwa makini. Utatumia huu mfano vilevile kwa kuhitimisha shughuli.

  • Kata umbo kubwa la balbu
  • Kata umbo la kasha la metali la balbu
  • Gundisha sehemu ya chini ya balbu kwenye pembe ya kulia ya pembe nne ili ienee kwenye eneo la pembe tatu lenye kivuli
  • Tumia chaki kubwa ya rangi nyeusi nyaya nene, kama inavyoonyeshwa
  • Tengeneza shanga ndogo yenye umbo la yai kutoka kwenye picha yenye rangi gazetini na ibandike kwenye mistari myeusi uliyoichora (hii inawakilisha shanga ya kioo ambayo huzuia nyaya mbili nene zisigusane)
  • Tengeneza filamenti kutoka kwenye mkunjo wa waya mwembamba, na ufunge; kukatisha ncha mbili za mistari minene myeusi. Njia mojawapo ni kushikisha ncha za waya uliojikunja kwenye kadibodi na kutumia upande usio sahihi wa utepe (wa nyuma) wenye gundi kuzifunga.
  • Kunja upande wa kushoto wa chini wa balbu kuelekea upande wa kulia. Sasa mfano wako wa balbu karibu unakamilika
  • Tumia matone ya Prestiki kuwakilisha alama za metali kwenye upande mmoja wa kasha, na chini ya ncha ya metali ya balbu.
  • Mwisho, uweke kivuli msambamba tenge kati ya ncha ya metali na betri. Hii inaonyesha tabaka jeusi la plastiki ambalo hutenganisha kasha la metali na ncha ya metali.

Mfano huu unatengenezwa hususani ili uweze kufafanua mpangilio wa sehemu za ndani za balbu. Kinachotokea ndani ya balbu yenye mwanga kitabaki kuwa ni kigeni kwa wanafunzi, labda wawe wamefikiria juu ya nini chaweza kutokea, na wakapata nafsi ya kuchunguza. Inawezekna kutumia msumeno wa kukatia chuma kwa makini kufungua kasha la metali la balbu kuukuu. Hapo mpangilio na mwelekeo wa nyaya vinaonekana vizuri.

Mfano wa balbu ya mwanga

Sasa waonyeshe mfano uliotengeneza wa balbu ya tochi. Uliza: Wanadhani wangegundua nini kama wangefungua kasha la metali? Nini kingekuwa ndani? Nyaya mbili zinaelekea wapi? Wape muda wafikirie.

Wanadhani mpangilio wa nyaya ambao umefichwa na kasha la metali utakuwaje?

Baada ya muda, unaweza kuufungua mfano wako na kuwaonyesha njinsi waya unavyojiunga na kwa lehemu kwenye kasha la metali, na jinsi mwingine unavyoenda kwenye ncha ya metali chini ya balbu ya tochi.

Sasa tumia mfano wako kufafanua kuwa kuna njia iliyokamilika, au saketi (mzunguko wa umeme) ya umeme pale balbu inapowaka. Umeme uko huru kusafiri katika njia iliyokamili. Unasafiri kutoka kwenye betri, kupitia waya hadi kwenye kasha la metali, halafu kwenye waya mmoja mnene. Kutoka hapo, unapitia kwenye filamenti ya waya mwembamba. Unasababisha filamenti iwake, na hurudi nyuma kwenye waya mwingine mnene hadi kwenye betri tena.

Imechukuliwa kutoka: Umthamo 3, University of Fort Hare Distance Education Project

Nyenzo-rejea ya 2: Njia salama za kuchunguza umeme