Nyenzo-rejea 4: Kadi za kazi

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

KADI YA KAZI 1: JOTO

Unakuwa na:

Betri ya tochi/balbu ya tochi

Waya mtupu mwembamba wa urefu wa sm 10 wa fyuzi 

Waya mtupu wa kawaida wa shaba wa urefu wa sm10

Unachofanya:

  • Shika waya wa sm 10 ncha zake moja ikiwa juu na nyingine chini ya betri.
  • Gusisha mkunjo wa waya nyuma ya kiganja cha mkono wa mtu. Anahisi chochote?
  • Rudia kwa kutumia waya mwembamba/au waya wa fyuzi. Anahisi kitu chochote sasa?
  • Hapa unahisi aina gani ya nishati?
  • Jadili juu ya ulichohisi. Jaribu kufikiria maelezo yako mwenyewe. Jaribu kwa kutumia nyaya tofauti kuwasha balbu. Linganisha ung’avu wa mwanga. Unafikiri nini?

KADI YA KAZI 2: USUMAKU

  • Unakuwa na:
  • Betri ya tochi
  • Waya wa shaba wenye urefu wa sm 30 uliofunikwa
  • Msumari mkubwa laini wa chuma
  • Baadhi ya vitu vya metali-pini,nk.
  • Unga wa chuma
  • dira ndogo

Unachofanya:

  • Kwanza angalia kama msumari mkubwa laini wa chuma una madhara yoyote kwenye pini, dira.
  • Kunja waya kuzunguka msumari mara nyingi.
  • Shikisha ncha mbili tupu za waya kwenye ncha mbili za betri
  • Wakati waya umejishikiza, angalia kama kuna madhara kwenye pini, n.k
  • Ni aina gani ya nishati unapata?
  • Unaweza kufanya ncha moja ya msumari isukume upande mmoja wa dira?
  • Nini maelezo ya kikundi chako juu ya ulichokiona hapa?

KADI YA KAZI 3: MWENDO

Unakuwa na:

  • Betri ya tochi
  • Waya wa shaba uliofunikwa wenye urefu wa sm 25
  • Pini ambayo ina usumaku (imefanywa kuwa sumaku kwa kuwekwa pamoja na sumaku kwa muda)
  • Kipande cha kadi nyembamba inayojikunja ya sm 15
  • Mota ndogo ya umeme inayotokana na mwanasesere aliyeharibika au redio
  • Pini ya kuchorea

Unachofanya:

  • Zungusha waya kwenye penseli kutengeneza mzingo.
  • Funga kipande cha kadi kwenye pembe ya meza/dawati ionekane kama ubao ya kuogelea kwenye bwawa la kuogelea.
  • Sukuma pini yenye usumaku ili ining’inie wima kwenye ncha moja ya kipande cha kadi.
  • Shika mzingo sawasawa huku pini ya usumaku ikining’inia katikati mwa mzingo.
  • Shika betri ya tochi huku ncha moja ya waya kutoka kwenye mzingo ikigusa sehemu ya chini ya betri.
  • Mtu mwingine hivyo hivyo anagusisha ncha ya pili ya waya upande wa juu wa betri.
  • Jadili kitu ulichoona kinatokea. Ni aina gain ya nishati unaipata? Nini maelezo ya kikundikuhusu mlichokiona?
  • Sasa, igeuze betri juu-chini na urudie zoezi hilo. Lakini kwanza TABIRI kitu utakachokiona.
  • Mwisho – tumia betri ya tochi kutengeneza mota ndogo ya umeme. Unazungusha kuelekea upande gani? Unaweza kubadilisha mwelekeo?
  • Unadhani mota ya umeme inahusiana na mizingo ya nyaya uliofunikwa na sumaku?

KADI YA KAZI 4: SAUTI

Unakuwa na: Betri ya tochi

Spika ndogo kutoka kwenye kifaa cha umeme kikuukuu kilichoharibika

Mchanga mkubwa/vipande vya nyaya zinazojikunja

Unachofanya:

  • Fanya jaribio kuona kama unaweza kupata sauti kutoka kwenye spika kwa kugusisha ncha za betri na spika (kwanini mara zote huwa mbili?).
  • Inakubidi uweze kupata sauti kali.
  • Unatakiwa ufanye nini ili sauti irudie?
  • Sambaza mchanga mkavu juu ya koni ya spika iliyo wazi. Unagundua nini unaporudia kutoa sauti kali?
  • Ziangalie spika kwa makini. Unaweza kuona mipangilio yoyote ya sumaku na mizingo au mizunguko ya nyaya?
  • Jadili mtazamo wako mwenyewe namna spika zinavyofanya kazi.
  • Unaweza kuunganisha mtazamo wako na kadi ya kazi 3: Mwendo?

KADI YA KAZI 5: MWANGA

  • Unakuwa na:
  • Betri tatu za tochi
  • Balbu nne za tochi
  • Nyaya za kukunjika zenye urefu mbali mbali
  • Tayari umeshaona jinsi tunavyowasha balbu na tayari umeshachunguza mfumo wa balbu ya mwanga.

Unachofanya:

  • Chunguza mipangilio mbalimbaIi ili upate idadi mbalimbali ya betri za tochi kuwasha idadi mbalimbali ya balbu.
  • Andika mipangilio mbalimbali inayofanikiwa. Chora picha kuonyesha mipangilio hiyo.
  • Ni balbu zipi zilitoa mwanga mkali sana?
  • Unaweza kufikiria kuelezea ulichokiona?

Nyenzo-rejea 3: Dhana ya kutathmini zana

Nyenzo-rejea ya 5: Dondoo za mwalimu