Sehemu ya 4: Kuuangalia mwanga na kivuli

Swali Lengwa muhimu: Kwa jinsi gani tunavyoweza kuchanganya sayansi na maeneo mengine ya mtaala.

Maneno muhimu: mwanga; kivuli; kuakisi; mfumo; kutathmini; kusubiri; uchunguzi

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Umewasaidia wanafunzi kufanya uchunguzi wao wenyewe;
  • Umewahamasisha wanafunzi wako kujenga ujuzi wa kisayansi wa kutabiri;
  • Umewahamasisha wanafunzi wako kujenga ujuzi wa kisayansi wa kutabiri;
  • Umejijengea ujuzi na kujiamini katika kuunganisha maeneo mbalimbali ya mtaala.

Utangulizi

Kama mwalimu wa sayansi, unatakiwa kuwasaidia wanafunzi wako kuviangalia kwa umakini vitu tusivyotilia maanani. Mwanga, giza, kivuli, rangi na uakisi ni sehemu kubwa ya maisha yetu ya kila siku, lakini tunatoa umuhimu mdogo kwa sayansi inayotumika.

Sehemu hii inaangalia namna mwanga unavyokuwa kwenye maumbo na vitu mbalimbali. Inapendekeza mbinu shirikishi za kujifunza ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa namna mwanga unavyotumiwa kwa malengo mbalimbali na wajijengee ujuzi wa utabiri. Pia inajenga mahusiano ya sayansi na sanaa na teknolojia. Hii itawasaidia wanafunzi kujenga uelewa wa matumizi ya sayansi.

Muhimu: Nyenzo Rejea 1: Ushauri wa Usalama kwa waalimu ina ushauri muhimu wa usalama unaohusiana na mada hii.

Nyenzo-rejea ya 6: Periskopu – fikra za kukuwezesha kuanza