Somo la 1

Anza kwa kuchunguza mwanga na kivuli mwenyewe, kwa kutumia picha kutoka magazetini au kwenye picha. Ni sehemu gani ya picha inayoonekana kwa kuwa iko kwenye mwanga? Ni wapi unapoona kivuli? Unaweza kutafuta chanzo cha mwanga kinapotoka? Ni lini tunapoona taswira ya umbo (dondoo nyeusi ya kitu au mtu)?Jaribu hili wewe mwenyewe au na wenzako.

Sasa unachunguza ‘chanzo’ na ‘madhara’ yanayohusiana na mwanga kwa kuzingatia ushahidi ulioshuhudia na kufikiri kisayansi. Unaweza kujaribu uchunguzi huu na baadhi ya wanafunzi wako.

Uchunguzi Kifani 1 unaonyesha namna ilivyo muhimu kwa wanafunzi kupata uzoefu wa sayansi wanayoizungumzia. Katika Shughuli 1, unawahamasisha wanafunzi wako juu ya madhara wanayoona na kufahamu taratibu wakati wa kufanya majaribio ya mwanga.

Uchunguzi kifani ya 1: Kategoria za Uwezekano

Busiku alikuwa anaenda kuwasomea wanafunzi wake hadithi juu ya mwanafunzi aliyepoteza kivuli chake. Kwanza, aliwaandaa watambue vivuli vyao kwa umakini. Nje kwenye jua la asubuhi waliviona vivuli vyao kwenye karatasi kubwa. Vivuli vilionyeshwa, vikakatwa kwa umakini, kuonyeshwa na kujadiliwa darasani na kwenye eneo la kukusanyikia.

Hadithi maarufu ya kivuli kilichopotea ilisomwa mara nyingi. Katika hadithi hii, mtoto anapoteza kivuli chake, lakini anatafuta njia ya kukipata tena. Mpaka sasa, vivuli halisi vilikuwa vimeharibika kidogo. ‘Ndiyo! ‘Ndiyo!’ Waliitikia kwa makelele Busiku alipowaambia warudie shughuli. Muda huu aliwapeleka nje mchana. Na wao pia walikuwa wanapoteza vivuli vyao! Wanafunzi walichanganyikiwa na kusikitikika. Kwa hekima, Busiku aliamua makusudi kuwaacha hivyo hivyo.

Kwa majuma machache yaliyofuata, darasa liliongelea uzoefu huu, kwa kulinganisha na ugunduzi mwingine. Taratibu walijenga uelewa wa kilichotokea kwenye vivuli vyao.

Shughuli ya 1: Kugundua kinachoweza kufanywa na mwanga na kivuli

Ukiwa na darasa lako, jadili mchezo wa kubuni unaochezwa usiku kwa kutumia mikono ili kutengeneza picha ya kivuli ukutani (angalia Nyenzo Rejea 2: Kivuli Ukutani ). Wape kazi ya nyumbani ya kutambua picha zinazoweza kutengenezwa.

Wanatakiwa wajue cha kufanya ili kujenga (chanzo) picha ya kivuli kuwa kubwa au ndogo (madhara).

Wanafunzi inabidi warudi kesho yake wakiwa tayari kuwasilisha walichopata.

Kuandaa namna wanafunzi watakavyo wasilisha vivuli vyao vya ukutani darasani.

Kuwasaidia kunakili walivyopata kwa:

Kuorodhesha picha walizowasilisha (wanafunzi wachore kuonyesha umbo la mikono;

Kuandika chanzo na madhara ya matokeo

Kama mtu akiitaja, waambie wachunguze kinachosababisha madhara kwamba baadhi ya picha zimefifia wakati zingine zinaonekana vizuri?

Mwisho,tumia vitu vya matumizi ya kila siku (kikombe, chanio, mkasi, nyundo nk.)ili kuandaa maswali. Wanafunzi wanatakiwa kuona picha tu siyo kitu halisi au namna kilivyoshikwa. Shika vitu tofauti kwa kuviachanisha ili kutoa kivuli cha kuvutia. Waambie wanafunzi wako kueleza hicho kitu ni nini na waeleze kwa nini wanafikiri namna hiyo.

Sehemu ya 4: Kuuangalia mwanga na kivuli