Somo la 2
Kuakisi kunachangia katika namna tunavyooona au kuufahamu mwanga na rangi. Kwa uhakika, bila kuakisi hatungeona kitu chochote (Angalia Nyenzo rejea 3: Habari kuhusu mwanga ili kujua zaidi juu ya vifaa na tabia ya mwanga.)
Kwenye sehemu hii, tunaangalia njia unazoweza kutumia kuwasaidia wanafunzi wako kutambua kinachotokea mwanga unapoakisiwa kwenye maumbo mbalimbali. Lengo lao lisiwe kuwapa majibu sahihi, bali uzoefu utakaowafanya watafakari na kuvutiwa na mada hii. Katika shughuli 2, Wahamasishe wanafunzi wako wachunguze kwa makini mifano ya kuakisi inayowazunguka. Uchunguzi Kifani 2 unaonyesha namna kazi moja ya mwalimu juu ya kuakisi ilivyowahamasisha baadhi ya wanafunzi kuwa wasanii wazuri.
Uchunguzi kifani ya 2: Kutafakari juu ya kuakisiwa kwa mwanga
Bibi Mosha anafundisha darasa la 5 & 6. Amekusanya kwa umakini na kujaza kadi za picha nzuri kutoka kwenye magazeti makuukuu ya lugha, kusoma na kuandika na kazi ya mawasiliano.
Aliposoma utangulizi wa sehemu ya kwanza, aligundua kwamba angeweza kutumia tena picha zake kwa ajili ya sayansi. Aliweza kuona aina mbalimbali ya kuakisiwa kwa mwanga ndani ya picha (siyo kivuli na usulisuli tu). Kulikuwa na kumetameta kwa mwanga juu ya maji, kuakisiwa kwenye kioo cha madirisha, kumeremeta kwa vitu vinavyong’aa pamoja na mng’ao kwenye ngozi ya koromeo. Aligundua kuwa hata mng’ao ndani ya macho ya mtu ni uakisi.
Kwanza, Bibi Mosha alilifafanulia darasa lake uhalisia aliojua juu ya mwanga na uakisi (angalia Nyenzo Rejea 3 ). Halafu, aliwapa picha waziangalie. Alishangazwa na namna walivyotambua maelezo mengi zaidi. Walikuwa na habari nyingi zaidi juu ya athari za mwanga juu ya maumbo mbalimbali. Kwa ujumla alishangazwa pale baadhi ya wanafunzi, waliokuwa wamevutiwa zaidi ya wenzake katika michoro, walianza majaribio ya kuchora uakisi wa vitu kwenye duara ili michoro yao kuwa halisi zaidi.
Shughuli ya 2: Kuchunguza uakisi na upinduaji wa vioo
Mchezo wa Kioo
Anza na mchezo huu. Kwa makundi ya watu wawili wawili, watoto waigize kama sura ya kioo ya mwenzake. Mwanafunzi mmoja anaongoza kwa umakini, na wengine wanafuatisha mwendo wa taratibu. Waache wanafunzi kufanya hivi kwa dakika chache.
Jadili uzoefu. Je, wanagundua kuwa kama kiongozi akikonyeza kwa jicho la kushoto, mfuasi (‘mirror image’) anakonyeza kwa jicho la kulia?
Upinduaji katika uakisi
Sasa tumia rangi ya mdomo au wanja ili kuweka alama kwenye mashavu na mikono ya baadhi ya wanafunzi. Andika ‘L’ au ‘R’ kwenye kiganja cha kila mkono na herufi ‘AB’ kwenye shavu lakulia na ‘OB’ kenye shavu la kushoto. Waache wachunguze watakachopata wanapojiangalia kwenye vioo halisi. Jadili uchunguzi wao.
(Shughuli nyingi zaidi kuamsha ari ya kukisia na kuchunguza vimedondolewa katika Nyenzo Rejea 4: Shughuli za uakisi za ziada )
Somo la 1