Somo la 3

Tunajaribu kuweka uhalisia wa dunia yetu kisha tunatumia tulivyopata ili kutusaidia kutenda.Hii ni sawa na Sayansi. Matokeo kutokana na uchunguzi yanaweza wakati mwingine kutumika kutatua matatizo tunayokumbana nayo maishani. Hapa ni kuhusianisha sayansi na teknolojia na inawasaidia wanafunzi kuelewa ni kwa nini ni muhimu kusoma sayansi.

Shughuli ya muhimu (isome sasa) imejengwa juu ya elimu iliyopatikana kutoka kwenye Shughuli 2 ili kutatua matatizo ya kiteknolojia. Utawapimaje wanafunzi wako kwa shughuli hii? Baada ya shughuli, fikiria jinsi wanafunzi wako walivyouchukulia ufanyaji kazi wa namna hii – Walifanya kazi vizuri ndani ya vikundi? Utafanya kitu kingine tofauti na hiki wakati mwingine utakapofanya hivi?

Katika Uchunguzi Kifani 3 , Mwalimu anawahamasisha wanafunzi wake kutumia walivyopata kutoka shughuli 1 kuandaa na kuwasilisha michezo ya kivuli cha kikaragosi.

Uchunguzi kifani ya 3: Mchezo wa kivuli cha kikaragosi

Bwana Mbuli alionyesha kivuli cha vitu visivyojulikana kwenye kioo wakati wa kufanya Shughuli 1. Wanafunzi watatu walibaki nyuma kuchunguza na kuchezea zana zilizotumiwa. Aliwaangalia alipokuwa anasafisha darasa. Waligundua kuwa mkasi au chamburo vilionekana kutamka ukisogeza sehemu zake.

‘Aisee, Mimi ni Bwana Mkasi-mdomo. Mimi ni mwepesi sana!’

‘Na mimi ni Bwana Nyundo Nzito naenda kukupiga mpaka ufe!’ Mara walitengeneza mtiririko wa mchezo mfupi ambapo Bwana Nyundo anamtishia Bwana Mdomo wa Mkasi. Lakini Bwana Mdomo wa Mkasi anaokolewa na Bwana mshikio mrefu wa Koleo! Bwana Nbuli anawapa nafasi ya kuwasilisha mchezo wa kivuli cha kikaragosi chao darasani.

Darasa limevutiwa na kivuli cha kikaragosi. Baadhi ya wanafunzi walitengeneza wahusika watokanao na kikaragosi na kugundua namna ya kuunganisha sehemu zinazoweza kujongea, kwa kutumia waya mwembamba au mabua ya majani makavu kwa ajili ya fito na nguzo. Jinsi walivyotumia kile walichojifunza kwenye sayansi kulimshanagaza Bwana Mbuli. Walivifanya vikaragosi vionekane vikubwa na vidogo, vionekane vizuri na vingine viwe na mikwaruzo, na waliweza kutengeneza maumbo mbalimbali kwa kutumia kikaragosi kimoja kwakukishikilia kwenye pembe mbalimbali za kioo. (Angalia Nyenzo Rejea 5: Mawazo ya kutengeneza kivuli cha kikaragosi .)

Shughuli muhimu: Utatuzi wa tatizo –kutumia mwongozo wa sayansi

Andika swali hili ubaoni:

‘Kuna tatizo gani kama wewe ni mtu mfupi uliyesimama nyuma ya kundi la watu kwenye mpira wa miguu?’

Huwezi kuona! Waeleze wanafunzi wako namna utakavyotatua tatizo lako? Vipi kuhusu vioo? Andaa kitu cha kutatua tatizo la kutoona vitu vilivyoko juu yako.

Katika kundi la watu watatu/wane, mtindo wa wanafunzi, huunda, utengeneza, ulinganisha na kupima vyombo vyao kuangalia kwenye kona au juu ya kitu kilichozuia juu.

Kabla hawajaanza, wanafunzi wanapaswa kujadili hoja zifuatazo kwenye makundi yao:

Utahitaji vioo vingapi?

Ni pembe zipi ambazo vioo vitahitajika ili viweze kuwekwa?

Ni namna gani utakavyoshikilia, kuchomeka au kuhimili vioo kwa usalama?

Chora mpango wa chombo hicho.

Halafu, wanafunzi waanze kujenga vyombo vyao, jadili nao

vigezo utakavyotumia kutathmini vyombo vyao. Chora orodha na iweke wazi wakati wa shughuli.

Nyenzo Rejea 6: Periscopu –mawazo ya namna unavyoweza kuanza yana mawazo yaliyopangiliwa kwa ajili ya periskopu na baadhi ya mapendekezo ya namna ya kutathmini

Nyenzo-rejea ya 1: Ushauri wa Usalama kwa waalimu