Nyenzo-rejea 3: Habari juu ya mwanga

Taarifa za msingi/ welewa wa somo wa mwalimu

Vyanzo vya mwanga

  • Jua-chanzo kikuu cha mwanga na joto hapa duniani.
  • Nyota-majua ya mbali. Tunaweza kuona mwanga wake lakini hatuhisi joto.
  • Mwezi na sayari-huakisi mwanga wa jua.
  • Mwanga wakati wa radi.
  • Moto, miale, cheche, vyuma vilivyoyeyushwa na kaa la moto
  • Mwanga wa umeme.

Rangi

Wakati mwanga mweupe unapopindishwa na sehemu zilizowazi, hata matone ya mvua, hugawanyika na kuonyesha rangi saba za upinde wa mvua.

Vitu vyenye rangi husharabu rangi nyingine na kuakisi rangi zake tu. Hivyo, gari la rangi nyekundu huakisi rangi nyekundu tu, kioo chekundu kwenye taa ya breki hutoa mwanga mwekundu tu.

Kusafiri kwa Mwanga

Hakuna kinachosafiri kwa kasi zaidi ya mwanga.

Kama sauti, mwanga husafiri kama mawimbi yenye nguvu. Tunaongelea mawimbi ya sauti, lakini mionzi au mwali wa mwanga ni zaidi.

Mionzi ya mwanga kwa ujumla husafiri kwenye mistari iliyonyooka inayotoka kwenye chanzo.

Tunaona vitu kwa vile mionzi ya mwanga inagonga kwenye vitu hivyo

(huakisiwa).

Giza ni kwa sababu ya kutokuwepo kwa mwanga. Kama hakuna chanzo cha mwanga kwa ajili ya kuakisi vitu tunaona giza na hatuwezi kuona chochote.

Nini kinatokea kwa mwanga unaosafiri?

Hupitia kwenye kitu kinachoonyesha (kioo, maji, plastiki inayoonyesha, n.k)

Hupitia kwa kiasi kwenye vitu visivyopitisha mwanga (karatasi nta, tishu, miwani iliyotiwa rangi, ukungu na mawingu, nk.).

Mwanga huzuiliwa na vitu visivyopenyeza nuru – hivi husababisha kivuli. Mwanga pia huakisiwa na vitu visivyopenyeza nuru.

Sehemu zenye kung’aa (vioo, chuma kilichong’arishwa, n.k) huakisi picha yenyewe/halisia.

Sehemu zilizofifia hutawanya mwanga unaoakisiwa. Mwanga usiposafirishwa au kuakisiwa, unasharabiwa.

Wakati mwanga wote unaposharabiwa na kitu chochote tunauona kama mweusi.

Sura kwenye kioo

Tunapojiangalia kwenye kioo, sura tunayoona inakuwa kama inatoka nyuma ya ya kioo. 

Sura ya kwenye kioo hubadilisha vitu kinyume. Hii ndiyo sababu hatuwezi kusoma kwa urahisi ukurasa ulioshikiliwa juu ya kioo.

Jaribu kushika mikono kwa kutumia sura yako kwenye kioo-utaona kwamba ukiushika mkono wa kulia, sura ya kwenye kioo itaonyesha upande wa pili ambao ni mkono wa kushoto.

Nyenzo-rejea ya 2: Vivuli vya Ukutani

Nyenzo-rejea 4: Shughuli za ziada za uakisi