Somo la 1

Wanafunzi wana mawazo yao juu ya tofauti kati ya usiku na mchana kwa kutumia uzoefu wao. Mawazo haya si lazima yafanane na ufahamu wa kisayansi. Kwa mfano, katika maisha ya kila siku, tunaongelea jua kuchomoza au kuzama, ikionyesha kana kwamba jua ndilo huzunguka na siyo dunia. Pamoja na hayo, kwa kutumia kifani rahisi, inawezekana kutia changamoto na kuyapanua mawazo ya wanafunzi na kuwasaidia kujibu swali: ‘Kwa nini tuna usiku na mchana?’

Shughuli 1 inatoa njia rahisi ya kuonyesha usiku na mchana na Uchunguzi Kifani 1 unaibua mawazo zaidi. Unaweza kujaribu shughuli hii na wenzako kwanza, kabla ya kuijaribu na wanafunzi. Hii itapima uelewa wako na kukusaidia kuamua njia nzuri ya kutumia kifani darasani kwako.

Uchunguzi kifani ya 1: Kuigiza usiku na mchana

Bi Abdul, anayefanya kazi na wanafunzi wa daraja la 6 kwenye shule ndogo ya kijijini Kaskazini mwa Sudan, alikuwa anatafuta mawazo ya wanafunzi wake juu ya usiku na mchana. Kwa ajili ya kazi ya nyumbani, aliwaambia wanukuu majibu waliyopata walipowauliza marafiki zao, walezi na wanajamii wengine maswali yafuatayo:

Kwa nini huwa kuna giza? Usiku na mchana vinatokeaje? Utaonyeshaje hivi kwa wengine? Siku iliyofuata waliwasilisha kile walichopata.

Bi Abdul aliwaonyesha njia ya ya kuigiza usiku na mchana. Alitumia mshumaa kama jua na kuwaomba wanafunzi kadhaa’ kujitokeza na kuwa Dunia na kurudi walikotoka taratibu. Walivokuwa wakigeuka, aliwauliza ni wakati gani waliweza kuona mshumaa. Walipogeuka kwa mara ya pili, aliwauliza nini ilikuwa mchana na usiku na ni lini ilikuwa mawio na machweo.

Waliongea juu ya njia zao za kuonyesha usiku na mchana na kulinganisha na kifani cha Bi Abdul na kujadili namna mawazo yao yanavyooana. Bi Abdul alishangazwa na idadi ya maswali ya usiku na mchana ambayo wanafunzi waliuliza, pia namna Kifani kilivyowasaidia kuelewa kilichokuwa kinaendelea.

Shughuli ya 1: Usiku na mchana

Ukifanya kazi na darasa zima, waambie wakueleze wanavyojua kuhusu namna usiku na mchana unavyotokea. Kubali na kunukuu kila wazo na kwa kila pendekezo andika jina la aliyelitoa. Mara mapendekezo yote yatakapokuwa yameorodheshwa, waambie wote kuonyesha ni wazo gani wanalounga mkono kwa kunyoosha mikono yao; halafu andika idadi pembeni mwake.

Tumia Nyenzo Rejea 1: Kuandaa usiku na mchana kukusaidia kuandaa kifani cha usiku na mchana kwa ajili ya darasa.

Waambie wanafunzi kuongea na majirani zao jinsi ya kuelezea usiku na mchana, na kunukuu mawazo yao.

Kupima uelewa wao, tumia Nyenzo Rejea 2: Dodoso Kuhusu Mchana na Usiku. Ungeweza kusoma maswali au kumuuliza mwanafunzi mmoja katika kila kundi kusoma maswali kwenye makundi yao. Waambie wanafunzi wanukuu majibu yao kisha shirikiana nao majibu haya mwishoni.

Sehemu ya 5: Kutoka ardhini kuenda kwenye nyota – kutumia zana kifani