Somo la 2

Wakati mwingine watu hurejea kwenye mwezi wanapoandika au kuongea:

wanatumia misemo kama ‘mara moja kwa mwezi’, ‘kupigwa na mwezi na

‘mwezi wa mavuno’. Ni misemo gani unayojua inatumia neno ‘mwezi’? Ni misemo gani ambayo wanafunzi wako wanajua? Hapa unaweza kuhusianisha na kazi zamaandishi.

Katika Shughuli 2, wanafunzi wako wachunguze kwa undani umbo la mwezi kwa majuma/wiki kadhaa. Kisha jenga juu ya uchunguzi huu kwa kutumia vifaa vya kawaida kuonyesha mabadiliko ya umbo la mwezi. Hili litawasaidia wanafunzi kuelewa mabadiliko ya umbo/sura ya mwezi. Jaribu sughuli ya sehemu ya model mwenyewe kabla ya kuitumia na wanafunzi wako. Kutumia hadithi fupi za asili juu ya jua na mwezi ni njia nyingine ya kuamsha ari ya wanafunzi. Unaweza kutumia hadithi zako fupi za asili badala ya zile zilizotumiwa katika Uchunguzi Kifani 2 .

Uchunguzi kifani ya 2: Sayansi, mwezi na usimuliaji wa hadithi

Bwana Lowassa aliamua kuwasomea hadithi wanafunzi wake wa darasa la

2 juu ya na mwezi ili kuamsha ari yao kabla hawajasoma mwezi kama

mada ya sayansi. Alitumia hadithi katika Nyenzo Rejea 3: Jua, Mwezi na Maji, inayoongelea juu ya jua na mwezi kama mke na mme waishio duniani. Wanafunzi wake walifurahia hadithi, hasa pale ambapo Bwana Lowassa aliwasomea kwa sauti mbalimbali za wahusika.

Baada ya kujadili hadithi hii, Bwana Lowassa aliwaambia wanafunzi wake kumweleza namna mwezi ulivyo angani. (Aliwakumbusha wanafunzi kutoliangalia jua moja kwa moja kwa sababu linaweza kuharibu macho yao.)

Alivuta mawazo yao na kuwaonyesha kifani vya maumbo/sura za mwezi alichotengeneza ili kuwasaidia kuelewa kwa nini mwezi una maumbo/sura tofauti tofauti.

Shughuli ya 2: Vipindi vya mwezi

Waulize wanafunzi wako, kama wanaweza, kuuangalia mwezi jioni wanapokwenda nyumbani na kutilia maanani kwenye umbo lake. Siku inayofuata wanafunzi wachore umbo la mwezi. Waulize kama mwezi una umbo kama hili kila wakati. Kama sivyo, kwa nini? Kama sivyo, unabeba maumbo gani mengine? Yako sawa? Kuna mpangilio wa maumbo?

Panga orodha ya wanafunzi watakaokuwa wanaangalia mwezi kila usiku kwa majuma kadhaa na wanukuu maumbo yake kwenye chati uliyotayarisha kwa ajili ya shughuli hii. Angalia mwishoni mwa Nyenzo Rejea 4: Mwezi na mahusiano yake na dunia na Jua) .

Baada ya mwezi, waambie wanafunzi wajadili na kujibu maswali yafuatayo:

Ni namna gani umbo la mwezi hubadilika kwa juma

Unalielezeaje umbo la mwezi? Kwa nini umbo linabadilika?

Kisha, wasaidie wanafunzi kujenga uelewa kwa kuandaa maumbo sura za mwezi kwa kutumia njia katika Nyenzo Rejea 1 kwa kutumia mipira au matope ili kuona namna mwezi unavyoweza kubadilisha umbo. Nyenzo Rejea 4 inakupa raarifa zaidi juu ya mwezi.