Somo la 3

Watu wamekuwa wakivutiwa na anga. Wanafunzi wengi wanavutiwa na anga, na anga la usiku ni udhihirisho kuwa kuna zaidi ya dunia yetu.

Kugundua mfumo wa sayari hakuwezi kufanywa kwa ziara za kishule. Lakini kwa kutumia vitabu, darubini, kompyuta, mtandao navifani. Unaweza kuonyesha upana na undani wa mfumo wa sayari kwa wanafunzi wako. Ukubwa ni kitu kinachowasumbua wanafunzi kuelewa, lakini kutengeneza vifaa vya kifani vya mfumo wa sayari kutasaidia.

Katika Uchunguzi Kifani 3 , Mwalimu anatumia masimulizi ya kwenye komputa, aina mojawapo ya kifani ili kusaidia kujenga uelewa wa wanafunzi. Kama unaweza kupata komputa ya kufanyia kazi hii, jaribu kutumia nyenzo iliyoonyeshwa mwishoni mwa Nyenzo Rejea 4. Uchunguzi kifani unaonyesha jinsi Mwalimu alivyoruhusu kila kundi la wanafunzi kupata nafasi kwenye kompyuta na sehemu iliyobaki ya darasa walifanyia kazi shughuli nyingine zinazohusiana na hili.

Katika Shughuli Muhimu , wanafunzi wako wanatumia vifani kuonyesha mpangilio wa sayari. Ungeweza kupanua kifani cha mfumo wa sayari kwa kuwaambia wanafunzi kutafuta muda ambao kila sayari inalizunguka jua na kurudi kwenye mhimili wake (mchana na usiku).

Baada ya hapo, rudi kwenye shughuli. Wanafunzi wako wanapokeaje utengenezaji wa vifani? Unafikiri vifani vimewasaidia kuuelewa mfumo wa sayari? Unaweza kutumia vifani kwa mada nyingine–Vipi kuhusu kuutenez vifani vya kuonyesha chembe chembe?

Uchunguzi kifani ya 3: Kutumia masimulizi ya mfumo wa sayari

Bi Mucaba alikuwa anafanya kazi na darasa lake la 5 lenye wanafunzi 46 katika Shule ya Msingi Usangi ili kugundua mfumo wa sayari. Alifungua kwenye kompyutasehemu ya mtandao ya shule, kifani cha masimulizi ya mhimili wa jua, Dunia na mwezi. (angalia Nyenzo Rejea 4 kama mfano).

Alitaka wanafunzi wake kutafuta majibu kwa baadhi ya maswali waliyokuwa wameuliza juu ya jua, Dunia na sayari nyingine.Maswali yalikuwa yameorodheshwa kwenye karatasi pembeni mwa kompyuta na makundi ya wanafunzi wanne au watano walijaribu kuyajibu kadri walivyotazama simulizi.

Sehemu ya darasa iliyobaki ilikuwa ikiandika shairi la hisia zao juu ya kuwa sehemu ya mfumo wa sayari, waliojadili kama darasa zima mwanzoni mwa kipindi.

Shughuli muhimu: Kuandaa Mfumo wa sayari

Anza kwa darasa lako kutafakari juu ya mfumo wa sayari (Angalia Nyenzo Rejea Muhimu: Kutumia ramani ya mawazo na kutafakari ili kutambua dhana.) Nukuu mawazo yao yote na maswali juu ya sayari, jua mwezi n.k.

Washirikishe wanafunzi wako habari za kina juu ya sayari kwenye Nyenzo Rejea 5: Mfumo wa sayari–kweli na takwimu. Waambie wanafunzi kufanya kazi kwenye vikundi vya watu

wawili wawili wachore mchoro kuonyesha kila sayari kwa mpangilio, wakitoa baadhi ya viashiria vya ukubwa wa kila sayari. Halafu kila kundi lishirikishe mchoro wao kundi jingine kuhakiki majibu yao.

Liambie kila kundi kutengeneza kifani cha sayari moja kwa kutumia udongo wa mfinyanzi. Kama unaweza kupata vitabu na/aumtandao wa intaneti vitumie ili upate habari nyingi zaidi.

Hakikisha kuwa vifani viko kwenye vipimo sawa.

Halafu, tumia vifani vya sayari kujenga mfano wa mfumo wa sayari. Utatakiwa kwenda nje kuvipanga vifani vyao vizuri. (Angalia Nyenzo Rejea 6: Vipimo vya Mfano wa mfumo wa sayari kwa dondoo za ukubwa na maeneo ya sayari kwenye kifani.)

Mwishowe, panga mkusanyiko na darasa lako. Wanatakiwa kuonyesha kifani chao na waiambie shule walichopata kwenye mfumo wa sayari.

Nyenzo-rejea ya 1: Kutengeneza usiku na mchana