Somo la 1

Wanafunzi wengi sana wanajua mengi kuhusu mazingira ya mahali pao na wanaweza kuchora welewa wao wa mahali vitu vilipo kwa namna yao wenyewe. Kwanza, ni muhimu kukuza uwezo wa wanafunzi wako katika kuchunguza mazingira ya mahali pao na kufanya shughuli hizi ziwe na manufaa kwao. Eleza kwamba kuona sura za mazingira katika maeneo yao yanayowazunguka kunawafanya watambue sehemu mbalimbali zinazomhusu kila mmoja wao na kuzielezea kwa ufasaha. Kuwa na dhana ya uelekeo kunawasaidia wanafunzi kufika sehemu mbalimbali kwa kutumia njia zao. Watakapofahamu mazingira yao wenyewe, na njia zao tofauti za kuyafikia, wanafunzi wako wanaweza kuanza kudadisi kuhusu mazingira ya ulimwengu yaliyo mapana zaidi.

Njia mojawapo ya kuchunguza mazingira ya mahali hapo ni kuwahimiza wanafunzi wako kutembea na daftari na kuchora au kuandika vitu vyovyote vinavyovutia wanavyoviona wanapotembea kuzunguka eneo la mahali hapo. Njia nyingine ni kufanya kazi na wanafunzi wako na kutengeneza picha ya darasa ya kuchora au ya kubandika kwenye ukuta wa darasa. Kila siku, wanafunzi wachache wanaweza kuongeza picha (na maneno kutoka kwa wanafunzi wakubwa) za vitu vilivyoko kwenye mazingira ya mahali hapo.

Katika Uchunguzi Kifani 1 , mwalimu mmoja anaonesha jinsi alivyolisimamia darasa kubwa. Soma Uchunguzi Kifani huu kabla hujajaribu Shughuli ya 1 .

Uchunguzi kifani ya 1: Ramani ya shule na mazingira yake

Bibi Kazimoto, mwalimu wa Shule ya Msingi Dabanga nchini Tanzania, anataka kukuza ujuzi wa wanafunzi wake wa Darasa la 3 katika kuchunguza na kubainisha sura muhimu za nchi katika eneo la mahali hapo. Baadaye ataendelea na uchoraji wa ramani.

Bibi Kazimoto ana darasa kubwa; kwa hiyo anawagawa katika makundi manane yenye wanafunzi kumi kwa kila kundi. Anafahamu kwamba utumiaji wa kazi za makundi utamsaidia kulimudu darasa na kuhakikisha kwamba wanafunzi wote wanashiriki. Vilevile, itawasaidia wanafunzi kukuza ujuzi wao wa ujifunzaji shirikishi. (Angalia Nyenzo rejea ya Muhimu: Utumiaji wa kazi za makundi katika darasa lako .)

Analiambia kila kundi kuoredhesha vitu vyote vilivyoko katika ardhi ya shule ambavyo huviona wakati wanapokuja shuleni, kama vile miti, majengo, n.k. Anamwambia mtu mmoja toka kila kundi kuandika taarifa zote muhimu. Baada ya dakika chache, analiambia darasa limalize shughuli hiyo na analitaka kila kundi lisome kwa sauti kitu kimoja toka kwenye orodha yao, ambacho anakiandika ubaoni. Anazungukia kila kundi namna hiyo mpaka makundi yote yanamaliza kusoma vitu vyote.

Kisha, Bibi Kazimoto analipatia kila kundi karatasi kubwa na kuwaambia wanakundi waweke umbo-mraba katika ya karatasi kuonesha shule. Halafu kila mwanafunzi anaambiwa aweke kitu kwenye karatasi katika mahali sahihi..

Baada ya kila kundi kumaliza kazi hiyo, Bibi Kazimoto anawatoa nje kwenda kuona kama walichoweka kwenye karatasi ni mahali sahihi na kama kuna kitu cha kukihamisha au kukiongeza. Michoro yao imeboreshwa na kisha inaoneshwa darasani.

Bibi Kazimoto anaona kwamba makundi mawili yamefanya vizuri sana. Makundi mengine yanatakiwa kubadili vitu vichache na anapanga kuwapeleka wanafunzi hawa nje kimakundi kuchora ramani rahisi zaidi ya ardhi ya shule na vitu vinavyoonekana.

Shughuli ya 1: Safari ya kuelekea shuleni –alama na ishara

Waambie wanafunzi wachunguze na kurekodi katika kijitabu chao au daftari lao vitu muhimu 6–10 wanavyoviona njiani wakielekea shuleni siku itakayofuata. Wanafunzi wa umri mdogo wanaweza kufanya kazi ya kuchora.

Darasani, mwambie kila mwanafunzi kupangilia alivyoviona kwa kufuata utaratibu wa cha kwanza kukiona mpaka cha mwisho kukiona.

Waeleze wanafunzi sura ya mandhari ni nini.

Waambie wanafunzi waweke tiki kwenye sura za mandhari katika orodha yao.

Waulize kwa nini baadhi ya vitu walivyovichunguza si sura za mandhari. Je, wanatarajia kuviona vitu hivi kwenye ramani? Jadili kwa nini iko hivi, kwa mfano, vitu vingine kama mbwa na paka vinatembea, kama yanavyotembea magari, kwa hiyo vitu hivi si sura za mandhari (za kudumu).

Waulize wanafunzi wanafuata uelekeo gani wanapokuja shuleni, yaani, Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi (Ksz, Ks, Ms na Mg). Unaweza kutakiwa kueleza kuhusu uelekeo na kuwa tayari na ramani kwa ajili ya kuwaonesha au kuwakumbusha kuhusu Ksz, Ks, Ms na Mg.

Kutokana na msingi wa uelekeo, unda makundi manne, kila moja liwe na wanafunzi wanaotoka takriban katika mwelekeo mmoja.Based on the directions, (Angalia Nyenzo rejea Muhimu: Utumiaji wa kazi za makundi katika darasa lako.) Ikiwa wanafunzi wako wote walikuja shuleni kutoka katika mwelekeo mmoja au miwili, tunashauri uwachukue wanafunzi wako katika matembezi ili kutalii mielekeo mingine.

Waambie kila kundi kutengeneza orodha ya pamoja ya sura za mandhari zilizopo kwenye njia yao kuelekea nyumbani. Je, wanaweza kuziweka katika utaratibu wa mfuatano ambapo wanaweza kuziona wakiwa njiani toka shuleni kwenda nyumbani?

Onesha orodha zote kwenye kuta za darasa, kulingana na uelekeo.

Unaweza kufanya shughuli gani nyingine za kukuza ujuzi wa uchunguzi kwa wanafunzi wako?

Sehemu ya 1: Uchoraji wa ramani kwa mazingira ya mahali hapo