Sehemu ya 2: Makazi na rasilimali

Swali Lengwa muhimu: Shughuli gani unaweza kutumia kutafiti sababu za watu kuishi katika sehemu fulani?

Maneno muhimu: nyenzo;uchunguzi kifani;kazi za kundi;makazi;mdahalo;maswali

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • umetumia kazi ya kikundi na mdahalo kusaidia wanafunzi kuelewa rasilimali zinazohitajika katika maisha;
  • umetumia picha na ramani kutafiti uhusiano baina ya rasilimali zilizopo na makazi ya watu.

Utangulizi

Kila siku ya maisha yetu tunatumia rasilimali za aina zote na kadili idadi ya watu duniani inavyongezeka na uhitaji wa rasilimali unaongezeka.

Kama mwalimu unayetafiti mawazo haya, ni muhimu kuanza kwa kutafiti nini tayari wanafunzi wanakifahamu kuhusu rasilimali katika mazingira yao. Sasa itawezekana kupanga namna ya kupanua ufahamu wao na kuwahusisha katika kufikiri kiundani kuhusu mada. Chunguzi kifani katika sehemu hii inaonesha baadhi ya walimu walielezea mawazo haya na itakusaidia kufikiria kuhusu utakachofanya katika shughuli hii.

Nyenzo-rejea ya 3: Maswali yanayohusu ramani