Somo la 1

Wakiwa njiani kuelekea shuleni, wanafunzi wako wataona rasilimali nyingi za asili zinazotumika katika maisha ya kila siku. Katika sehemu hii utawauliza wanafunzi ku pendekeza baadhi ya rasilimali hizi na namna watu wanavyozitumia. Kwa kuzipanga kutegemeana na umuhimu wake kwa watu wanaoishi mazingira fulani, wataona jinsi rasilimali hizi zilivyo muhimu. Hii itawasaidia wanafunzi wako kukuza ujuzi wa kuchunguza na kufikiria kuhusu matumizi yake; pia katika kutumia rasilimali kwa busara. Utahitaji kutafiti ufahamu wao wa utofauti baina ya rasilimali asili na rasilimali zilizotengenezwa na watu.

Utatafuta pia njia za makundi katika kuliongoza darasa. Kufanya kazi kwa namna hii kutawasaidia kushirikishana mawazo na kujifunza pamoja.

Soma uchunguzi kifani1 kabla ya kujaribu shughuli 1: hizi zinaonesha njia mbalimbali za kutafiti wanachojua wanafunzi. Unaweza kujaribu njia zote kwa nyakati tofauti ukiwa darasani.

Uchunguzi kifani ya 1: Uchunguzi wa rasilimali tunazohitaji kwa maisha na maendeleo

Nchini Tanzania, wanafunzi wengi wanatoka vijijini. Bwana, Kaizilege ni mwalimu katika shule ya msingi Kitahya, iliyo karibu na kijiji cha Ileme, Tanzania.

Kijiji kipo katika mazingira ambayo yana rasilimali asili kama miti, maji, na mashamba yanayolimwa. Bwana Kaizilege anategemea kuendeleza uwezo wa wanafunzi katika kuchunguza na kutambua rasilimali halisi katika mazingira yanayozunguka kijiji chao. Anategemea hili litawasaidia kuelewa kazi na wajibu wao katika matumizi kulingana na rasilimali hizi za asili.

Mwishoni mwa siku aliwataka wanafunzi kuorodhesha rasilimali zote walizoziona kijijini wakirudi nyumbani na kuleta orodha shuleni. Siku inayofuata aligawanya wanafunzi katika makundi ya watu nane na kuandika swali lifuatayo ubaoni

Ni rasilimali gani tunazo katika mazingira yetu?

Mwanafunzi kutoka kila kundi hunukuu swali katika kipande cha karatasi na kila kundi hushirikisha utafiti kutoka siku iliyopita ya zoezi la utafiti, kuchora au kuandika matokeo kuhusu swali. Bwana Kaizilege huonyesha matokeo ubaoni na kwa pamoja huakisi namna mawazo yao yanavyofanana. Bwana Kaizilege hujaza nafasi zilizopo kwenye jedwali. Kwa mfano, hakuna aliyetaja jua au machimbo ya kokoto.

Bwana Kaizilege anaandika sentensi ubaoni. Kila sentensi inaonyesha matumizi ya rasilimali moja inayopatikana kwenye kijiji; Kisha aliwataka wanafunzi katika makundi kulinganisha kila sentensi na rasilimali. Makundi hushirikishana mawazo na kufikia makubaliano kabla ya kunakili kwenye madaftari yao.

Shughuli ya 1: Kutambua rasilimali za mahali na kutafiti umuhimu wake kulingana na mahitaji

Andika ‘rasilimali mahali’ katikati ya ubao. Hakikisha wanafunzi wanafahamu kuhusu maana ya rasilimali. Watake wanafunzi kutumia dakika tatu kuongelea kuhusu rasilimali wanazotumia katika kijiji.

Halafu, watake jozi tofauti za wanafunzi kutoa mawazo.

Andika mawazo yao katika orodha mbili ubaoni-‘Rasilimali asili’ na ‘Rasilimali zilizotengenezwa na watu’.

Sasa gawanya darasa katika makundi madogo na waeleze kila kundi kujadili baadhi ya tofauti baina ya rasilimali asili na zile zilizotengenezwa na watu.

Watake kila kundi kutoa majibu yao kwa darasa. Jadili pamoja na darasa dondoo muhimu walizotoa.

Waamuru kila kundi kupanga orodha ya rasilimali zote zinazopatikana katika kijiji chao, kutoka zile muhimu sana kwa jamii hadi zile zenye umuhimu kidogo.

Litake kila kundi kuwasilisha na kutetea mpangilio wao kwa wanadarasa wengine.

Kama darasa, kubaliana na orodha moja. Unaweza kuamua kwa kutumia kura

Watake wanafunzi kufikiri kuhusu rasilimali zinazopatikana na rasilimali ambazo ni ngumu kuzitunza/kuhifadhi au ni za gharama.

Je wanafunzi waliona utofauti kati ya rasilimali asili na zile zilizotengenezwa na binadamu? Kuna yoyote anahitaji msaada zaidi?

Sehemu ya 2: Makazi na rasilimali