Somo la 2

Watu kwa kawaida wamekuwa wakiishi sehemu ambazo wanaweza kupata rasilimali asili kama maji, kuni na urahisi wa kupata chakula, labda ardhi kwa ajili ya kulima mazao au kufuga ng’ombe au kuvua samaki kutoka ziwani au baharini.

Kusaidia wanafunzi kuelewa kwanini watu wanachagua sehemu fulani kwa kuishi, utatumia mfano wa kihistoria kutafuta masuala ya maji. Unaweza husisha mawazo muhimu na maisha yao ya kila siku.

Kwa kutumia kazi za kikundi utaongeza mijadala ambayo itawasaidia wanafunzi kutafiti fikira zao na kupanua zaidi ufahamu wao.

Uchunguzi kifani ya 2: Matumizi ya historia ya mwanzo ya Tanzania

Bibi Byabato alikuwa anafundisha darasa la 6 kuhusu uhusiano kati ya rasilimali asili na makazi ya watu. Aliamua kutumia mfano kutoka Tanzania ya zamani.

Aliandaa baadhi ya makala kuhusu Tanzania katika siku za zamani na aliandika historia hiyo ubaoni. (Rejea Nyenzo 1: Rasilimali asili na makazi ya watu Tanzania.) aliwaamuru wanafunzi katika jozi kutambua rasilimali kuu za asili zilizopo Tanzania na kujadili kwa nini watanzania huishi sehemu mbalimbali. Walikuwa na uwezo wa kutambua umuhimu wa maji kama rasilimali asili katika kuamua wapi waishi nchini

Halafu, aliwataka wanafunzi kutengeneza makundi ya watu nane na kila kundi kujadiliana juu ya umuhimu wa maji katika vijiji vyao. Aliwataka watambue wapi vijiji vinapata maji na namna maji yanavyoathiri maisha ya watu. Makundi yalishirikishana tafiti zao na wanafunzi wengine na Bibi Byabato aliandika mawazo yao ubaoni. Walijadiliana kuhusu umuhimu wa kila wazo.

Bibi Byabato alifurahishwa sana na majadiliano yaliyoonesha ufahamu wa wanafunzi-hii ina maana kuwa walielewa uhusiano kati ya rasilimali asili na makazi ya watu.

Shughuli ya 2: Kuhusianisha rasilimali na makazi

Gawanya darasa katika makundi na watake kila kundi kufikiri kuhusu mahitaji na wakazi (mfano maji,chakula na malazi). Mwite mwanafunzi mmoja kutoka kila kundi kuorodhesha mawazo ya kikundi.

Litake kila kundi kufikiri ni sehemu gani ingekuwa nzuri kwa makazi mfano karibu na mto lakini mbali na maeneo yanayoweza kukumbwa na mafuriko.

Litake kila kundi kuwasilisha utafiti wake kwa wanafunzi wengine na kutambua sababu zinazolingana na makundi mengine.

Halafu, kila kundi lifikiri na kuandika shughuli ambazo zinazoweza kuwa zilifanywa na watu wengine katika makazi haya.

Sasa litake kila kundi kubuni vijiji vyao. Lipe kila kundi kipande kikubwa cha karatasi. Waambie waonyeshe:

mto nyumba

eneo lenye mwinuko;

barabara

Wahamasishe kutumia alama kwenye ramani na kujumuisha maumbo mengine kadili wanavyo taka.

Toa muda mwishoni mwa kipindi kwa makundi kuwasilisha ramani za vijiji na kueleza ambako watu katika kijiji wanapata rasilimali.