Somo la 3

Rasilimali nyingi ni haba na hivyo zinahitaji kutunzwa vizuri. Baadhi ya rasilimali, mara zikitumika, haziwezi kubadilishwa. Nyingine ni nyingi kwa sasa lakini zinaweza kuisha kama hazikutumika vizuri.

Katika uchunguzi kifani 3, mwalimu hutumia mdahalo wa darasa kutafiti rasilimali ulani. Kama unawanafunzi wakubwa unaweza kujaribu njia hii, chagua mada yoyote inayoelekeana na jamii yako. Mafanikio ya mdahalo yatategemea muda waliopewa wanafunzi kupanga mdahalo wao vizuri na kuwaandaa wanafunzi ili wajue majukumu yao katika mdahalo huo.

Katika shughuli muhimu, utawahamasisha kutumia njia nyingine ya kutafiti rasilimali katika eneo lao.

Uchunguzi kifani ya 3: Mdahalo juu ya matumizi ya rasilimali

Bibi Masawda aliwataka wanafunzi wa darasa la sita katika mkoa wa Usambara kutafiti faida na hasara za matumizi ya rasilimali asili. Aliamua kuitisha mdahalo darasani juu ya suala kilimo cha kufyeka na kuchoma, kinachotokea sehemu nyingi duniani.

Alianza kipindi kwa kuandika ubaoni madhara ya kilimo cha kufyeka na kuchoma kwa mazingira.

Halafu Bibi Masawda alielezea namna mdahalo unavyofanya kazi (Rejea Nyenzo 2: Namna ya kudahalisha mada) aliwataka wanafunzi atatu kukubali mada na wanafunzi wengine watatu kutokukubali mada. Alielezea kwa makundi yote kuwa wanatakiwa kutoa ushahidi kujenga hoja zao. Kuwasaidia kupata ushahidi alihamasisha kila kundi kuongea na wazee katika jamii juu ya kwa nini wakulima wanatumia njia ya kufyeka na kuchoma katika kuandaa mashamba. Pia aliwapa baadhi ya taarifa alizozipata kwenye mtandao zinazozungumzia kufyeka na kuchoma na baadhi ya matokeo yake kwenye mazingira.(Rejea Nyenzo 3: Kilimo cha kufyeka na kuchoma)

Aliwapa muda wa majuma mawili kujiandaa kwa mdahalo ikijumuisha muda wa kipindi kwa wanafunzi wote kufikiri juu ya faida na hasara za kuchoma misitu. Wanafunzi wengine walijaribu kutafiti kile walichoweza kutoka kwa jamii yao na kushirikishana na pande zote mbili za mdahalo. Siku ya mdahalo, Bibi Masawda aliwakumbusha wanafunzi taratibu za mdahalo na umuhimu wa kuuliza maswali kama hawakuelewa.

Mwishoni mwa mdahalo, kura zilipingwa na mada iliamuliwa kutokana na kuungwa mkono na wengi. Bibi Msawda aliwakumbusha wanafunzi kuwa ilikuwa muhimu kuheshimu kila mawazo ya wanafunzi na sio kushangilia kuwa ‘Washindi’. Alifurahishwa na makundi yote kwa kutoa mawazo yakuvutia ikiwa kukubali au kupinga mada

Katika kipindi kilichofuata, Bibi Masawda aliwataka wanafunzi kutoa mawazo kuhusu kukuza uelewa wa jamii juu ya madhara ya kuchoma misitu na kuwapa njia mbadala za kutumia ardhi katika jamii yao. Aliandika mawazo yake ubaoni na kuwahamasisha wanafunzi kujadili mawazo hayo na familia zao.

Shughuli muhimu: Kulinganisha maeneo

Chagua moja ya maelezo yaliyopo kwenye Nyenzo 4 Mazingira tofauti na ubandike darasani. Kama unapicha zilipigwa ziarani sehemu tofauti za Tanzania au kama unaweza kupata maelezo katika kitabu au magazeti unaweza kutumia. Jaribu kuchagua sehemu iliyotafauti sana na mazingira ya shule.

Waeleze wanafunzi picha ni ya wapi

Wapange katika makundi ya wanafunzi watatu au wane na watake kufikiri kati ya maneno manne hadi sita ya kuelezea eneo

Baada ya dakika tano, litake kila kundi kutoa neno moja. Andika maneno hayo ubaoni au kwenye karatasi

Halafu watake wanafunzi kufanya kazi katika makundi yao na kuorodhesha maumbo ya eneo hili yanayofanana na yanayotofautiana na mazingira yao.

Nyenzo-rejea ya 1: Rasilimali asili na Makazi ya watu Tanzania