Nyenzo-rejea ya 1: Rasilimali asili na Makazi ya watu Tanzania

Nyenzo za mwalimu kwa kuandaa au kubadili kwa matumizi ya wanafunzi

Kutoka siku za nyuma hadi leo, mfumo wa makazi ya watu umekuwa ukisababishwa na upatikanaji wa rasilimali asili. Chakula maji na makazi ni mahitaji muhimu ya binadamu na zinaonesha uwezo wa kustawi au kutostawi kwa jamii katika mazingira iliyopo. Jamii za zamani kama Lakoja ziliishi mabondeni ambako zilikuwa na uhakika wa kupata chakula na maji na pia zilipata njia za usafikiri kibiashara. Vile vile, ulinzi na matumizi bora ya rasilimali hatimaye yalionesha namna jamii ilivyojiimarisha na uwezo wa kuzitunza rasilimali kwa vizazi vijavyo

Moja ya tatu ya watanzania hupata chini ya milimita 800 za mvua, na hivyo ni jangwa au nusu jangwa. Moja ya tatu tu ya nchi inapata mvua zaidi ya mm 1000. Hata hivyo asilimia 7 ya ardhi ya Tanzania ni maziwa. Hii inajumuisha ziwa Viktoria (ziwa la pili kwa ukubwa duniani lenye maji yasiyo ya chumvi) ziwa Tanganyika (ziwa la pili kwa kina kirefu duniani) na ziwa nyasa. Maziwa ya ndani ni Rukwa, Eyasi na Manyara. Pia kuna mito mikubwa inayotiririsha maji kwenye maziwa. Watanzinia walioishi zamani wangeanzisha mfumo wa kilimo cha umwagiliaji kutoka kwenye vyanzo hivi vya maji wangezalisha zaidi mazao yao. Kwa mfano wachagga walianzisha mtandao wa umwagiliaji kwa kutumia mifereji au mfongo ambayo inakusanya maji kutoka vijito vya Kilimanjaro na kupeleka eneo la mashambani

Nyenzo-rejea 2: Namna ya kudahalisha maada