Nyenzo-rejea 2: Namna ya kudahalisha maada

Nyenzo za mwalimu kwa kuandaa au kubadili kwa matumizi ya wanafunzi

Mdahalo ni majadiliano yaliyo rasmi. Upande mmoja unapinga mada na mwingine una kubaliana na mada. Kunawazungumzaji wakuu wa tatu kila upande na kuna muda maalumu ambao wanatakiwa kuwasilisha mitazamo yao. Mdahalo ni shughuli rasmi na ina taratibu Fulani ambazo lazima zifuatwe.

  • Mwenyekiti huanzisha mada na wazungumzaji sita.
  • Mzungumzaji wa kwanza kutoka kundi linalikubali mada huzungumza kwanza. Mzungumzaji wa kwanza huanzisha mada wanaweza kuongea kwa muda uliopangwa (kwa mfano, dakika 3 hadi 5 kila mmoja)
  • Halafu, mzungumzaji kutoka kundi linalopinga mada huzungumza. Mzungumzaji huyu pia huanzisha mada lakini kutoka upande wa wanaopinga.
  • Wanafuatiwa na wazungumzaji wa pili kutoka kila upande. Majukumu ya mzungumzaji wa pili ni kuendeleza mawazo kwa kutoa mifano halisi na ushahidi kushadidia mtazamo wa upande wake.
  • Mwenyekiti hufungua mdahalo kwa watu wengine ambao huweza kuuliza maswali kwa mzungumzaji kutoa changamoto juu ya mawazo.
  • Mzungumzaji wa tatu kutoka upande unaopingana na mada hutoa majumuisho ya mawazo ya kundi.
  • Mzungumzaji wa tatu kutoka upande wa wanaokubaliana na mada hutoa majumuisho ya mawazo ya kundi. Darasa hupiga kura juu ya mada, kuzingatia uzito wa mawazo yaliyojadiliwa.

Nyenzo-rejea ya 1: Rasilimali asili na Makazi ya watu Tanzania

Nyenzo-rejea 3: Kilimo cha kufyeka na kuchoma