Nyenzo-rejea 3: Kilimo cha kufyeka na kuchoma

Nyenzo za mwalimu kwa kuandaa au kubadili kwa matumizi ya wanafunzi

Nini maana ya kilimo cha kufyeka na kuchoma?

Kilimo cha kufyeka na kuchoma ni pale ambapo msitu wa asili au wa kupandwa unapochaguliwa na kukatwa uoto wote kuruhusu ukauke. Miti mikubwa mara nyingi hubanduliwa magana kuruhusu ikauke ikiwa imesimama. Baadhi ya miti huachwa imesimama hasa ile inayoonwa kama ni muhimu kama miti inayozalisha chakula au ni muhimu kiuchumi. Sehemu ya miti hukatwa kuwa mbao au hukusanywa kutumika kama kuni na kutengeneza mkaa. Baada ya muda (juma ama mwezi) mabaki yaliyokauka huchomwa. Sehemu hiyo hulimwa mwa muda mchache (kwa kawaida mwaka mmoja hadi mitano) halafu inaachwa kwa kuwa rutuba imeisha na mazao hayawezi kustawi na magugu huota.

Mashamba haya yaliyoachwa mara nyingi hutumika kama malisho ya mifugo. Kama shamba limeachwa lioteshe uoto, malisho yatakuwa ni kwa muda tu. Hivyo misitu mara nyingine huachwa iote yenyewe kwa lengo la kufyeka na kuchoma kwa mara nyingine siku za usoni.

Uchomaji huondoa uoto na unaweza kutoa virutubisho vitakavyorutubisha udongo. Majivu pia huongeza kipimo cha Haidrojeni ya udogo mchakato unaofanya baadhi ya virutubisho( hasahasa fosiforasi) viwe vinapatikana kwa muda mfupi. Uchomaji pia huua muda wadudu wa ardhini, wadudu na mimea iliyokuwepo muda mrefu na kuwa majivu ambapo mazao mapya hupandwa. Kabla ya mbolea za chumvichumvi hazijawepo, moto jamii nyingi zilitumia moto kurutubisha ardhi.

Kilimo cha kufyeka na kuchoma huhitaji eneo lenye watu wachache au kuendelea kupata eneo jipya, kwa vile misitu kurudia katika hali yake ya zamani inaweza kuhitaji miongo au hata kizazi na kizazi. Katika misitu mingi ya kitropiki njia endelevu za kufyeka misitu na kuchoma zimekuwa zikitumika kwa miaka mingi, lakini ongezeko la watu na kukua kwa sekta ya viwanda kumefanya ukataji na uchomaji asilia usiwe endelevu na

Ingawa ni njia panda kwa nchi za tropiki zilizo na wingi mkubwa wa watu, kilimo cha kujikimu kinaweza kuwa ni njia nyepesi ya kulisha familia zao. Matokeo ya hukataji na kuchomaji misitu kwa mfumo wa ikolojia ni mbaya unapotumika kwa kiasi kikubwa. Kinachoathirika sana ni udongo usio na rutuba, unaopitisha maji kirahisi katika misitu ya kitropiki. wakati mboji imeondolewa hata kwa kuvuna kuni au mkaa-mabaki kwenye udongo huathiriwa kwa kiasi kikumbwa hivyo kuathiri uoto wa aina yoyote. Mara nyingine kuna mizunguko mingi ya ukataji na uchomaji misitu ndani ya mwaka mmoja; kwa mfano, mashariki mwa Madagaska jambo lifuatalo hujitokeza mara kwa mara. Katika hatua ya kwanza inaweza kukata miti yote kwa matumizi ya kuni au kujengea. Miaka michache baadae miti michanga iliyoota huvunwa kwa ajili ya mkaa, na miaka michache baadae shamba huchomwa kurutubisha haraka ardhi kwa ajili ya kuotesha nyasi za mifugo. Kama mashamba ya jirani yametengenezwa kwa mtindo unaofanana na huu, mmomonyoko wa udongo huweza kutokea kwasababu hakuna mizizi au hifadhi ya maji ya muda katika matawi kupunguza mtiririko wa maji juu ya uso wa dunia. Kwa jinsi hiyo kiasi cha virutubisho vilivyosalia ardhini vinasafishwa. Eneo hili ni mfano wa jangwa na hakuna uoto wowote unaoweza kuota kwa karne nyingi zijazo

Urudishaji hali ya kawaida wa mfumo-ikolojia wa mandhari ya hapo juu umekuzwa zaidi kwasababu misitu ya tropiki ni makazi ya mifumo-ikolojia mchanganyiko, ulio na idadi kubwa ya aina ya viumbe vinavyoelekea kupotea. Kwa hiyo madhara ya kukata na kuchoma mimea ni makubwa kwa sasa duniani.

Imenukuliwa kutoka: Wikipedia Slash and Burn, Website

Misitu ya malagasi yarudi hali yake

Taarifa kutoka shirika la habari la Uingereza-BBC

Madagaska inapoteza kwa haraka misitu. Lakini wanavijiji wanakasirishwa na hatua zinazowazuia wao kukata miti katika hifadhi zilizotengenezwa hivi karibuni.

Madagaska ni kisiwa kikubwa katika bahari ya Hindi sehemu iliyosheheni aina 200000 za mimea na wanyama-robo tatu yake hazipatikani popote duniani na ni matokeo ya miaka mingi ya madadiliko tangu kisiwa kijitenge kutoka Afrika wakati mabara yanaundwa kwa mara ya kwanza.

Vilima vimefunikwa kwa misitu minene ya kijani iliyoenea kila kona. Miti hutanda juu kwa namna ya pekee kuzuia uoto chini yake. Anga hufunikwa na aina mbalimbali za ndege wa rangi tofauti.

Kakini si muda mrefu ambapo mandhari yatabadilika kuwa kame, yasiyo na uoto. Sehemu nyingine mmomonyoko wa udongo ni mkubwa unaoacha makorongo kwenye kingo za vilima.

Mimea michache sana humea hapa na hakuna wanyama.

Hii lazima ifike mwisho

Wanamazingira wanasema kilimo cha kukata na kuchoma -ambapo misitu hukatwa na kuchoma kusafisha kwa kupanda mazao-inaharibu misitu yakipekee na kuhatarisha maisha ya wanyama waishio humo.

‘Hii ni njia yetu ya maisha. Kama hatukati miti, hatuwezi pata chakula’. Dimanche Dimasy, mzee wa Mahatsara.

Katika mkutano wa dunia wa mazingira, uliokaa Afrika kusini mwaka

2003, Raisi Marc Ravalomanana alifurahishwa na wanamazingira na aliahidi kuongeza zaidi hifadhi ya rasilimali za Madagaska kutoka m1.7 hekta hadi m6 hekta ifikapo mwishoni mwa mwaka 2008.

‘[Kuna] kuna ujumbe mzito kutoka serikalini na kutoka kwa raisi mwenyewe ambaye anafuatilia hili na kuweka misingi,’ asasema Helen Crowley, mkurugenzi wa chama cha kuhifadhi mali asili-New York

Amelinganishwa na [raisi wa zamani wa Marekani] Teddy Roosevelt mwanzoni mwa karne iliyopita, ambaye aliona maliasili (misitu) ya nchi ikiharibiwa na kusema “Hii lazima ikome”.

Uchomaji misitu kizazi na kizazi

Lakini wafanyakazi wanasema kutekeleza mipango ya kuhifadhi mali asili katika kisiwa ambacho robo tatu ya wakazi wanaishi katika umasikini wa kutupwa itakuwa vigumu.

Serikazi imekwisha weka ramani kwa maeneo inayotaka kuyahifadhi na imeanza kuzungumza na jamii za mahali kabla ya kuwakataza kukata miti.

Hatua kadhaa zimekwisha chukuliwa kuhamasisha jamii ziishizo vijijini kuhusu umuhimu wa kutunza misitu

Lakini nilipoenda kutembelea hifadhi iliyotengenezwa hivi karibuni, ambamo kilimo cha kukata na kuchoma kimekatazwa, sikuona ushahidi wa watu wa mahali hapo kujulishwa.

“Kijiji chetu kimekuwa kikichoma misitu kulima mpunga kizazi na kizazi. Halafu wanakuja na kutuambia haturuhusiwi kufanya tena”. alisema Dimanche Dimasy, mzee wa kijiji cha Mahatsara, kilichopo ndani mwa hifadhi ya misitu ya mashariki mwa Mantadia.

‘Hii ni njia yetu ya maisha. Kama hatukati miti, hatuwezi pata chakula’.

‘‘Serikali inataka kuzuia misitu lakini hakuna mtu anayewajali na kuwatetea wakulima waishio hapa’

Wanamazingira wanasema kuna faida za muda mrefu kwa masikini kama watahifadhi misitu kama ardhi itatunza maji na virutubisho. Udongo ambapo miti imekatwa humomonyoka haraka, kupelekea isitumike, hivyo kuhitaji sehemu nyingine kusafishwa

Mahitaji ya kila siku

Lakini maafisa wa serikali wanasema kushawishi jamii za wakulima kuhusu umuhimu wa kutunza misitu ya Madagaska kunahitaji kubadilika kifikra.

‘Siyo kazi rahisi kubadili fikra za wakulima waishio vijijini’. Sylvain Rabotorison, waziri wa mazingira

Watu wanapokuwa masikini wanafikiri tu mahitaji yao ya kila siku’, anasema waziri wa mazingira, Sylvain Rabotorison

‘tunahitaji kuwaelimisha watu juu ya kwanini kutunzamazingira. Lakini siyo rahisi kubadili fikra za watu waishio vijijini-ina maana kubadili baadhi ya tabia za kizamani zisizo na tija.’

Yaweza maanisha pia kutafuta kitu mbadala kwa wao kufanya.

Mipango iko mbioni kuwafundisha njia bora za kilimo cha mpunga kinachoongeza mavuno lakini kinachotumia ardhi kidogo, na makundi ya utunzaji mazingira yanatoa majiko yanayotumia mkaa kidogo hivyo kupunguza ukataji miti.

Lakini mengi yanategemea kama faida za muda mfupi zinaweza kuletwa kwa watu masikini wa madagaska.

Bila ushirikiano wao, ahadi ya Raisi Ravalomanana itakuwa vigumu kufanikiwa.

Imenukuliwa kutoka chanzo : BBC World, Website

Nyenzo-rejea 2: Namna ya kudahalisha maada

Nyenzo-rejea 4: Mazingira tofauti