Sehemu ya 3: Kuchunguza hali ya hewa

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kufanya ujifunzaji wa hali ya hewa kwa upana na kwa vitendo zaidi?

Maneno muhimu: kutatua tatizo, hali ya hewa, kazi ya kundi,mpangilio, uchunguzi, kuchangia mawazo

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Umejenga uwezo wa wanafunzi wa kuchunguza, kukusanya data na utambuzi wa mpangilio wa hali ya hewa ili kuweza kutabiri hali ya hewa;
  • Umetumia kazi za makundi kuhimiza ushirikiano wakati wanafunzi wanapobuni na kuandaa vifaa vya hali ya hewa.

Utangulizi

Kwa watu walio wengi, kufuatilia hali ya hewa ni sehemu muhimu ya maisha ya kila siku. Kwa mfano, wakulima wanahitaji kutambua wakati muafaka wa kupanda mazao yao na wavuvi nao wanahitaji kujua ni wakati gani waingie baharini. Mlolongo wa hali ya hewa unatofautiana katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara, na vipindi vya mvua na vikavu navyo vinatofautiana. Ukiwahimiza wanafunzi wako kuchunguza mabadiliko ya mpangilio huo-hata yakiwa kidogo-kutawasaidia kuelewa uhusiano uliopo kati ya hali ya hewa, watu na mazingira yao.

Katika sehemu hii, utatumia kazi za makundi kujenga uwezo wa wanafunzi wa kushirikiana na kufikiria. Utapanga shughuli kwa vitendo ili kuhimiza ushirikiano kati yao.

Nyenzo-rejea 4: Mazingira tofauti