Somo la 1

Kuna imani nyingi na mashairi juu ya hali ya hewa katika sehemu mbalimbali duniani, ikiwemo Afrika. Kwa kutumia hivi kama kianzio cha kuchunguza hali ya hewa kutasisimua shauku ya wanafunzi wako ya kujua hali ya hewa ya mahali hapo na kuwahimiza kuwa makini na kukabiliana na mabadiliko katika mazingira yao ya asili. Kwa mfano, Nigeria, watu wa kabila la Yoruba inasemekana waliamini kuwa radi ni mzimu wenye nguvu ambao ulibeba nguvu za kichawi. Mzimu huo uliwakaripia kwa kutumia moto wa mwanga uliotoka mdomoni mwake. Uchunguzi kifani 1 unaonyesha njia moja ya kutumia misemo ya mahali hapo na wanafunzi wako

Ufundishapo kuhusu hali ya hewa, una utajiri wa nyenzo nje ya darasa lako. Kwa kuwaambia wanafunzi wako wakusanye data za hali ya hewa na kuangalia mpangilio katika data kwenye Shughuli 1, utakuwa umewahimiza wajijengee ujuzi wa kuchunguza.

Uchunguzi kifani ya 1: Kutumia elumu ya mila na desturi katika kujadili hali ya hewa

Bi. Ogun kutoka Abeokuta Nigeria alitaka kuwafundisha wanafunzi wake juu ya hali ya hewa na aliamua kuanza kwa kuwataka wamwambie walichokuwa tayari wanakifahamu kuhusu mada hiyo. Siku moja kabla ya kuanza mada hiyo, aliwaambia wanafunzi wake waulize familia zao na ndugu zao juu ya mashairi yoyote waliyokuwa wanajua yanayohusu hali ya hewa na kuyaleta shuleni.

Siku iliyofuata, aliwaambia wanafunzi wawili au watatu kuimba mashairi waliyopata Pia aliandika ubaoni mila na desturi chache zinazohusu hali ya hewa kutoka sehemu nyingine za Afrika (angalia Nyenzo rejea 1: Elimu ya Mila na desturi za Kiafrika juu ya hali ya hewa , zinazohusu maelezo ya kisayansi) na akajadili maana zake, ambazo si za kisayansi.

Halafu, aliwauliza ni kwa nini walidhani kuwa kuna mila na desturi tofauti zinazohusu hali ya hewa. Wanafunzi wake walitoa ushauri kuwa watu wa zamani hawakuelewa sababu za mabadiliko ya hali ya hewa na kwa maana hiyo, walibuni mila na desturi ili kuelezea mabadiliko hayo;

Bi. Ogun aliwauliza wanafunzi wake kwanini walidhani kuwa ni lazima kuelewa mpangilio wa hali ya hewa. Wanafunzi walishauri mawazo yafuatayo , ambayo aliyaandika ubaoni:

Kujua nguo za kuvaa. wakulima kujua mpangilio wa hali ya hewa, ili wapande mbegu, na kuvuna kwa wakati muafaka wa mwaka.

Kujipanga kwa ajili ya maafa ambayo yangeweza kutokea kutokana na hali ya hewa mbaya.

Aliwaambia wanafunzi wafanye kazi katika makundi ya watu sita, na kwa kutumia moja kati ya mawazo ya ubaoni,wabuni hadithi fupi inayohusu hali ya hewa. Baadhi ya wanafunzi waliandika hadithi zao na wengine waliamua kuziigiza darasani.

Shughuli ya 1: Jedwali la hali ya hewa,utabiri na mabadiliko ya hali ya hewa

Mwambie kila mwanafunzi arekodi joto, hali ya anga, mvua na kasi ya upepo (marambili kwa siku) mabadiliko ya hali ya hewa kwa muda wa siku tano mfululizo. (Angalia Nyenzo rejea muhimu 2: Jedwali la uchunguzi wa hali ya hewa ). Wanafunzi watahitaji kutumia kati ya dakika tano hadi kumi, wakati uleule kila siku nje ya darasa kufanya uchunguzi na kujaza majedwali yao. Kwa wanafunzi wadogo, unaweza kuwapa baadhi

ya maneno yatakayoweza kuwasiadia kuelezea hali ya hewa, kwa mfano, upepo mkali, upepo mwanana, na hali tulivu.

Waonyeshe wanafunzi wako jinsi ya kusoma kipima joto na kurekodi hali ya joto ( kama huna kipima joto, waambie wakadirie hali ya joto, kama vile joto sana,vuguvugu n.k)

Mwishoni mwa wiki, waambie wanafunzi wakae kwenye makundi ya watu sita na walinganishe data zao walizokusanya. Zinashabihiana kwa kiasi gani? Kuna tofauti yoyote? Kama zipo, wanadhani zimesababishwa na nini? (Angalia Nyenzo rejea muhimu: Kufanya kazi kwa makundi darasani kwako .)

Halafu, waambie wabashiri hali ya hewa ya wiki inayofuata na warekodi utabiri wao kwa ajili ya kuonyeshwa darasani. Waambie watoe sababu za ubashiri wao.

Rekodi hali ya hewa ya wiki ijayo kama ilivyokuwa awali. Mwishoni mwa wiki,angalia hali halisi ya hewa ukilinganisha na ubashiri wao. Jadiliana nao ni kwa jinsi gani walikuwa sahihi, na namna gani wangeweza kufanya utabiri wao uwe sahihi zaidi.

Sehemu ya 3: Kuchunguza hali ya hewa