Somo la 2

Sayansi ya kujifunza hali ya hewa inaitwa metorolojia. Wana metorolojia hupima joto, mvua, mgandamizo wa hewa, upepo, hali ya unyevunyevu angani n.k. Kwa kuangalia data na mpangilio wanaopata, wanatabiri jinsi hali ya hewa itakavyokuwa siku za usoni. Hii ni muhimu kwa ajili ya kuwapa watu kiashirio mapema cha hali mbaya ya hewa kama vile mafuriko na

pepo za baharini, pia utabiri ni wa msaada sana kwa watu wengine kama wakulima.

Sehemu hii inapeleleza jinsi gani kutumia watalaamu wa mahali hapo kunaweza kuleta mvuto kwa wanafunzi na kuonyesha njia na uhalisia wa kujifunza hali ya hewa. Shughuli 2 inatumia kutatua tatizo kama mbinu ya kuwasaidia wanafunzi kufikiri zaidi juu ya hali ya hewa.

Kama unaishi eneo lenye mvua za uhakika, ungeweza kuwaambia wanafunzi waandae kitu cha kupima mvua kila siku kwa muda wa majuma mawili.

Uchunguzi kifani ya 2: Kutembelea kituo cha hali ya hewa

Bi Mboma alikuwa na bahati kwa kuwa kulikuwa na kituo cha hali ya hewa kilomita chache kutoka shuleni na aliweza kuandaa safari. Wiki chache kabla ya kutembelea huko, na baada ya kuwa ana ruhusa kutoka kwa mwalimu mkuu na kuwaeleza wazazi, aliwapigia simu watu wa kituo cha hali ya hewa ili kupanga tarehe na kuwaeleza nini angependa kufanya. Mhusika alikubali kuliongoza darasa kuzunguka kituo hicho, kuwaonyesha vifaa na kuelezea matumizi yake. Bi Mboma alimweleza kuwa darasa lilikuwa limeanza kujifunza juu ya hali ya hewa na lilikuwa na uelewa mdogo sana wa vifaa vya kupima hali ya hewa.

Kabla ya safari, Bi Mboma aliwaambia wanafunzi wake walichokuwa wanategemewa kufanya, walichotakiwa kwenda nacho na nini wangetakiwa kufanya ili kuhakikisha usalama wao wakiwa safarini.

Kituoni, wanafunzi waliona vifaa mbalimbali vya kupima hali ya hewa, ikiwa ni pamoja na kipimahewa, kipimamvua na vifaa vya kupima upepo. Bi Mboma aliwahimiza wanafunzi wake waulize maswali mengi. Kwa msaada wa afisa wa kituo, walijaribu kutumia baadhi ya vifaa. Vile vile waliweza kuangalia baadhi ya rekodi na kuona mpangilio wa hali ya hewa. Afisa alimpa Bi Mboma baadhi ya nakala za data ili atumie darasani.

Waliporudi darasani, Bi. Mboma aliwaambia kila kundi la wanafunzi sita wafikirie ni jinsi gani wangeweza kuunda kituo chao kidogo cha hali ya hewa na namna gani wangeweza kuchukua vipimo sahihi. Makundi yakatengenezwa na darasa zima likaanza kazi.

Somo liliisha kwa darasa kutoa ahadi ya kuihusisha jamii kuanzisha kituo chao cha hali ya hewa.

Shughuli ya 2: Kupima upepo

Kwanza kabisa tengeneza propela na kipimaupepo. Hii inaweza kufanyika kwa kutumia vifaa rahisi na ungeweza kuomba msaada kutoka kwa mtu kutoka kwenye jamii ambaye anaweza kutengeneza. Ni vizuri kutumia muda mwingi kwa ajili ya hili kwa sababu vifaa vya kufundishia vinaweza kutumiwa na mwalimu mwingine na katika miaka ijayo (angalia Nyenzo rejea 3: kupima upepo na kasi yake kwa maelekezo ya kutengeneza hivi vifaa).

Toa tatizo la kutatuliwa na wanafunzi wako. Waulize, ‘unadhani kuwa upepo uko sawa katika viwanja vyote vya shule? Unawezaje kutambua?’

Waache waliongelee hili kwenye makundi yao kuhusu kuchunguza hili.

Wazungukie na kusikiliza maelezo yao, ukiwauliza maswali kama itaIazimu. Tumia maswali kama ‘Ungeweza kusimama wapi ili kuhisi upepo mkubwa?’ ‘Ungeweza kusimama wapi ili kuhisi upepo mdogo?’

Hakikisha kwamba kila kundi limeandaa mpango.Huu lazima uwe na matumizi ya mahali mbalimbali kuzunguka shule.

Mpango wa kila kundi unapokuwa tayari, waruhusu wakafanye uchunguzi. Ungeweza kuwapeleka nje kundi moja baada ya jingine. Inabidi warekodi uchunguzi wao kwenye jedwali (angalia Nyenzo rejea 4: Jedwali la uchunguzi ) kwa mfano).

Jadili matokeo na darasa zima:

Ni sehemu gain hapa shuleni unafikiri zina upepo mkubwa? Ni sehemu gain ya ya shule ina upepo mdogo?

Kwa nini kuna tofauti kati ya maeneo haya?

Waulize wanafunzi wako namna gani wangeweza kuona hali hiyo kwa mwaka mzima.