Somo la 3

Wakati ni rahisi kukusanya data za hali ya hewa darasani kwa kipindi fulani, si rahisi kuchunguza madhara ya hali ya hewa kwa kipindi kirefu.

‘Tabia ya nchi’ huelezea mpangilio wa hali ya hewa wa mahali fulani kwa kipindi cha miaka mingi.

Njia moja ya kuwasaidia wanafunzi kuchunguza madhara ya muda mrefu ya hali ya hewa yaweza kuwa kutumia hadithi, kama Uchunguzi kifani 3 unavyofanya. Hapa, wanafunzi wanaweza kufikiri juu ya mambo mapana zaidi. Nini kingeweza kutokea kama hali fulani ya hewa ingeendelea? Shughuli muhimu inatumia njia nyingine. Wanafunzi wanahimizwa kufikiri juu ya matatizo yanayoweza kutokana na hali ya hewa.

Uchunguzi kifani ya 3: Kuangalia madhara ya hali ya hewa kwenye maisha ya watu mbalimbali

Bi Mboma na wanafunzi wa darasa lake la tano walikuwa makini kuchunguza namna hali ya hewa ingeweza kuathiri watu na nyenzo nyingine katika njia tofauti. Aliamua kulihadithia darasa hadithi kwenye Nyenzo rejea 5: Namna gani hali ya hewa ilimwathiri Bwana Hoja na familia yake .

Alipokwisha kusoma hadithi yake kwa wanafunzi wake, Bi Mboma aliwapanga katika makundi, baadae akawapa mlolongo wa maswali.

Ni aina gani za hali ya hewa ambazo familia ya Bwana Hoja ilikumbana nazo?

Kwenye hadithi hii, hali ya hewa imebadilika mara ngapi?

Ni kwa vipi mkulima, Bwana Hoja, alijisikia kutokana na mvua kuongezeka ghafla?

Mvua ilikuwa na madhara gani kwenye mazao ya Bwana Hoja?

Unadhani ukosefu wa mvua katika eneo lake ungesababisha madhara gani kwa familia ya Bwana Hoja?

Ungejisikiaje kama ungepatwa na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyoelezwa kwenye hadithi hii?

Mwalimu Mboma alimwambia mwanafunzi mmoja kutoka kwenye kila kikundi kuandika dondoo kutoka kwenye majadiliano yao ili kutoa mawazo ya kikundi kwa darasa zima mwishoni mwa muda wa majadiliano.

Shughuli muhimu: Kuchunguza hali mbaya ya hewa

Changia mawazo na wanafunzi wako juu ya mifano ya hali mbaya ya hewa, kama vile, tufani, ukame, mafuriko, baridi sana, pepo kubwa.

Jadiliana na wanafunzi juu ya nini hutokea kwa kila janga. Ligawe darasa lako katika makundi. Waambie kila kundi kuchukua mfano mmoja wa hali mbaya ya hewa.

Itabidi wajaribu kufikiri juu ya matatizo ambayo hali hii ya hewa ingesababisha na kuyaandika kwa ufupi kuonyesha jinsi maisha yangeathirika.

Wape wanafunzi muda wa kutosha na wahimize watengeneze hiyo taarifa. Uliza maswali kama vile ‘Nini kingetokea kwenye mgawanyo wa maji?’ ‘Je kungekuwa na nishati? Chakula?’

Nyenzo-rejea ya 1: Jdi ya Afrika kuhusiana na hali ya hewa, nyenzo rejea ya mwalimu