Nyenzo-rejea ya 1: Jdi ya Afrika kuhusiana na hali ya hewa, nyenzo rejea ya mwalimu

Nyenzo za mwalimu kwa kuandaa au kubadili kwa matumizi ya wanafunzi

Nchi au eneo na aina ya hali ya hewaKiasiliMaelezo ya kisayansi
Africa: RadiJadi: watu waliopigwa na radi walidhaniwa na waafrika wa zamani walio wengi kuwa ni kwa ajili ya hasira za miungu. miale ya radi ilifikiriwa kuwa ni‘miale ya haki’.Sayansi: Radi hutokea pale ambapo umeme unasafiri kati ya maeneo mkabala yenye chaji ya umeme kwenye wingu, kati ya mawingu au kati ya wingu na ardhi. Miale ya radi kutoka kwenye wingu hadi ardhini (miale ya haki) inaanza kwa elektroni (chembechembe ambazo zimechajiwa asi (negative)) zikishuka kwa mwendo wa kuyumbayumba kutoka kwenye wingu, na zinatengeneza utepe wa ayani zilizochajiwa chanya kutoka ardhini.Ayani na elektroni zinapokutana, wimbi kubwa la chaji chanya husafiri kwenda juu kwaumbali wa kama km 96,000 (kama maili 60,000) kwa sekunde! Mchakato huu unaweza kurudia mara kadhaa kwa kipindi cha nusu sekunde, na hivyo kufanya radi ionekane kama inawaka.

Ethiopia:

upepo

Jadi: watu wengi waliamini kuwa mapepo mabaya yaliishi katika pepo zivumazo, hivyo wangeweza kuufukuza upepo kwa visu.Sayansi: Upepo unasababishwa na mkusanyiko wa nguvu changamani. Kupata joto na kupoa kwa hewa, husababisha mabadiliko ya uzito, au mgandamizo. Hewa huwa ina tabia ya kusafiri kutoka kwenye maeneo yenye mgandamizo mkubwa kwenda kwenye maeneo yenye mgandamizo mdogo. Hata tofauti ndogo ya mgandamizo kutoka eneo moja na lingine, inaweza kusababisha upepo wenye nguvu kuvuma. Msuguano kutoka kwenye vitu kama miti, milima na majengo huathiri upepo, hupunguza kasi yake, hutengeneza mawimbi, vikwazo n.k. Pia, kuzunguka kwa dunia hutengeneza kile kinachoitwamadhara ya Koriolisi ambapo pepo za kaskazini mwa ikweta hupinda kulia na zile za kusini mwa ikweta hupinda kushoto.

Misri:

Jua

Jadi: wamisri wa kale, wakisafiri kutumia mto Nile, waliamini kuwa jua lilisafiri kukatisha anga kwa kutumia mtumbwi usio na kina kirefu.Sayansi: Wakati jua linaweza kuwa linasfiri kukatisha anga, ni sisi ambao tunatembea kwenye uso wa nchi, kadri dunia inavyozunguka kwenye mhimili wake na kulizunguka jua. Mzunkuko mmoja huchukua masaa 23 na dakika 56, au siku moja na mzunguko mmoja wa kulizunguka jua huchukua siku 365.26, au mwaka mmoja wa kalenda.

Kenya:

Ngurumo za radi

Jadi: Mungu wa ngurumo za radi, Mkunga Mburu, anaaminika kusafiri katika mbingu kwa kutumia ng’ombe dume mkubwa mweusi akiwa na mkuikiradi kwenye mikono yake yote, tayari kuitupa mawinguni ili itoe sauti kubwaSayansi: Kelele tunazoita “Ngurumoza radi”- zinatokana na hewa iliyopata joto la zaidi ya nyuzi 43,000 °F wakatiradi inawaka ngurumo zinaongezeka na baadae taratibu kupungua radi inapoacha.

Nigeria:

Radi

Jadi: Wayoruba inasemekana kuwa waliamini kuwa radi ilikuwa ni mzimu wa dhoruba ambao ulibeba nguvu kali za uchawi. Mzimu uliwakemea kwa kutumia miale ya moto ya radi kutoka mdomoni mwake. Iliaminika kuwaadhibu watu kwa matendo yao mabaya kwa kuwaharibia vitu vyao ardhini au kwa kumpiga mtu kwa miale yake ya mwanga.Sayansi: Radi hutokea pale ambapo umeme unasafiri kati ya maeneo mkabala yenye chaji ya umeme kwenye wingu, kati ya mawingu au kati ya wingu na ardhi. Miale ya radi kutoka kwenye wingu hadi ardhini (miale ya haki) inaanza kwa elektroni (chembechembe ambazo zimechajiwa kinegative) zikishuka kwa mwendo wa kuyumbayumba kutoka kwenyewingu, na zinatengeneza utepe wa ayani zilizochajiwa chanya kutoka ardhini.Ayani na elektroni zinapokutana, wimbi kubwa la chaji chanya husafiri kwenda juu kwa umbali wa kama km 96,000 (kama maili 60,000) kwa sekunde! Mchakato huu unaweza kurudia mara adhaakwa kipindi cha nusu sekunde, na hivyo kufanya radi ionekane kama inawaka.

Afrika za kusini mashariki:

Upinde wa mvua

Jadi: Wengi wa wazulu wa zamani walifikiri kuwa upinde wa mvua ni nyoka aliyekunywa maji kutoka madimbwi ya maji ya ardhini. Kutokana na hii hadithi, nyoka huyu angeweza kuishi kwenye dimbwi lolote ambalo alikuwwa anakunywa na kummeza yeyote ambaye angetokea kwenda kuoga kwenye dimbwi hilo.

Sayansi: Pinde za mvua zinatokana na mvua. Matone ya mvua huwa kama vimche vidogodogo yanapopigwa na jua, huupindisha mwanga wa jua na kuugawa katika rangi tofauti. Upinde wa mvua huonekana kutoka angani hadi kukutana na uso wa nchi. Ili kuuona upinde wa mvua, ni lazima uwe umesimama jua likiwa nyuma yako, ukiiangalia mvua inanyesha kutoka upande mwingine wa anga. Upinde wa mvua unaweza kumaanisha kuwa mvua inaelekea kwisha, kwa sababu jua lazima liwe linachomoza kupitia mawinguni ili upinde uonekane.
Imenukuliwa kutoka chanzo: NASAhttp://scijinks.jpl.nasa.gov/ weather/

Nyenzo-rejea 2: Jedwali la unchunguzi wa hali ya hewa