Nyenzo rejea 3: Kupima mwelekeo na kasi ya upepo

Nyenzo za mwalimu kwa kuandaa au kubadili kwa matumizi ya wanafunzi

Kutengeneza kipimo cha mwelekeo wa upepo

Utahitaji:

  • Pini iliyonyooka
  • Kipande cha kadi
  • bua
  • mkasi
  • penseli yenye kifutio
  • utepe

Fanya hivi:

1. Kata kichwa na mkia wa mshale kutoka kwenye kipande cha kadi.

2. Zifunge kwenye ncha mbili za bua.

3. Kandamizia pini katikati ya bua.

4. Chomeka pini kwenye kifutio cha penseli. Hakikisha kuwa bua linaweza kuzunguka bila kikwazo.

Chanzo halisi: Galaxy Net, Website

Kutengeneza anemometa kwa ajili ya kupima kasi ya upepo

Anemometa ni kifaa kinachokueleza kasi ya upepo unaovuma. Anemometa halisi itaweza kupima kwa usahihi zaidi. Mfano uliotengeneza unaweza kukupa mwelekeo wa kasi ya upepo unaovuma, lakini hautakuwa sahihi kama anemometa yenyewe.

Unahitaji:

1. mkasi

2. vikombe vidogo vya karatasi

3. kalamu

4. vipande viwili vigumu vya kadibodi-vyenye urefu sawa

5. pini ya kuchorea

6. fimbo

7. udongo wa mfinyanzi kidogo

8. saa inayoonyesha sekunde

Fanya hivi:

1. Kata ncha za vikombe vya karatasi zilizojikunja ili kuvifanya viwe vyepesi.

2. Paka rangi kikombe kimoja kwa nje kwa kalamu ili uweze kukiona kila kinapozunguka.

3. Pishanisha vipande vya kadibodi ili vitoe alama ya (+). Vishikishe pamoja na uweke alama katikati.

4. Chomeka au pigilia mpishano wa kadibodi juu ya fimbo.

5. Puliza vikombe kuhakikisha kuwa kadibodi inazunguka sawasawa.

6. Uweke udongo wa mfinyanzi nje, kama vile kwenye ukingo wa miti, ukuta au mwamba. Chomeka ncha kali ya penseli kwenye udongo isimame wima.

Kupima kasi ya upepo:

Kwa kutumia saa, hesabu idadi ya mizunguko ya kikombe chenye rangi katika dakika moja. Unapima kasi ya upepo kwa kutumia idadi ya mizunguko kwa dakika. Anemometa ya watabiri wa hali ya hewa hubadili hii kasi kuwa maili kwa saa (au kilkomita kwa saa).

Nyenzo-rejea 2: Jedwali la unchunguzi wa hali ya hewa

Nyenzo rejea 4: Jedwali la uchunguzi