Nyenzo rejea 5: Ni jinsi gani hali ya hewa ilimwathiri Bwana Hoja na familia yake

Nyenzo za mwalimu kwa kuandaa au kubadili kwa matumizi ya wanafunzi

Bwana Hoja ni mkulima na ni mkuu wa familia yenye watoto sita.

Siku moja, familia ya Hoja iliamka kwenye hali ya hewa safi na ya jua. Wakiwa njiani kwenda shambani, mtoto mdogo kuliko wote alikuwa akilalamika kuwa jua kali, na alivua shati lake kwa sababu ya joto.

Kipindi cha mchana, wakati kila mtu alikuwa anafanya kazi shambani, mvua ilianza kunyesha.Kila mtu alilowa kwa maji ya mvua na waliacha kufanya kazi hadi hapo mvua ilpoacha kunyesha kwa muda kama wa saa zima. Wakati huo, mtoto mdigo alikuwa akifurahia mabadiliko ya hali ya hewa na alikimbia shambani akicheza na maji na majani ya miti.

Baada ya mvua, watoto ghafla waligundua kuwa joto lilikuwa limepoa. Hii hali iliwahamasisha kufanya kazi kwa masaa mengine mawili kabla hawajaondoka kurudi nyumbani.

Bwana Hoja hakuwa anategemea mvua siku hiyo na hivyo hakuwa na furaha kwa sababu mvua ilimharibia mipango yake ya siku hiyo shambani, lakini alimshukuru Mungu kwa kuwa mvua ingeboresha mazao yake.

Usiku ule, hali ya hewa ikawa ya baridi sana na familia ilibidi iwashe moto mkubwa na kuuzunguka ili kupasha miili yao joto kabla ya kwenda kulala.

Nyenzo rejea 4: Jedwali la uchunguzi

Sehemu ya 4: Utafiti wa mabadiliko wa Mazingira