Sehemu ya 4: Utafiti wa mabadiliko wa Mazingira

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kukuza upeo wa masuala ya rasilimali na uchafuzi wa mazingira?

Maneno muhimu: mazingira; tafiti kundi; ziara; rasilimali; ongezeko la joto; uchafuzi

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • umetumia njia tofauti kukuza ufahamu juu ya uchafuzi na mabadiliko ya hali ya hewa.;
  • umetumia mbinu za utafiti kusaidia wanafunzi kupeo kuelewa madhara ya uchafuzi;
  • umetumia kazi za makundi na ziara rahisi kukuza ufahamu wa wanafunzi juu ya rasilimali asili.

Utangulizi

Ukuzaji wa ufahamu wa wanafunzi wako kuhusu mazingira yao na hitaji la kulinda na na kuhifadhi mazingira ni muhimu katika kuelewa majukumu yao ya kutunza mazingira kwa ujumla. Sehemu hii inalenga kukusaidia kuandaa kipindi na shughuli zitakazo husisha kuifadhi mazingira ya mahali fulani na matatizo ya uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Kuwasaidia wanafunzi wako, unatakiwa kusoma kuhusu masuala ya mazingira. Hii itakupa mchango wa mawazo kuhusiana na kipindi na kukufanya uwe na mtazamo wa kisasa.

kadili wanavyohusishwa na shughuli zenye maana kwao kwa kutafiti masuala kama uchafuzi wa mazingira katika maisha halisi na kwa kufanya majaribio, wanafunzi wako watafurahia kujifunza,

Nyenzo rejea 5: Ni jinsi gani hali ya hewa ilimwathiri Bwana Hoja na familia yake