Somo la 1

Wanafunzi wako wanajua nini kuhusu rasilimali za mahali? Sehemu hii inahusu kuongeza ufahamu wa wanafunzi wako juu ya rasilimali asili- hasahasa mimea inayopatikana kwenye maeneo yao.

Njia nzuri ya kufanya hivi ni kukusanya wataalam wa maeneo hayo kuzungumzia juu ya rasilimali asili kama ilivyo katika uchunguzi kifani 1. Wataalamu huleta elimu fulani ambayo wewe na wanafunzi wako mtajifunza. Kutumia wataalamu hufanya ujifunzaji uwe wa kusisimua kwa sababu ni tofauti na ilivyozoeleka.

Katika shughuli 1, unapanua upeo wa wanafunzi wako wa mazingira yao kwa kutumia ziara za kimasomo ambapo wanahusishwa kikamilifu katika ukusanyaji wa taarifa. (kama unafanyia mazingira ya mjini au kama mazingira siyo salama kwa wanafunzi kutembea, unaweza kubadili shughuli na kuangalia chakula sokoni. Mtake kila mwanafunzi kutaja majina matano ya vyakula vinavyotokana na mimea na kujaribu kutafiti wapi vinazalishwa.)

Uchunguzi kifani ya 1: Kutafiti rasilimali muhimu za mahali

Bibi Hlungwane hufundisha shule ya msingi Hoxane iliopo mji wa Limpopo Afrika Kusini na huwataka wanafunzi wake kupanua ufahamu wao kuhusu mazingira na rasilimali asili zake. Alisoma kuhusu wataalamu wa mahali na elimu kuhusu mimea ya dawa, na anafikiri kuangalia mimea ya mahali hapo, ikijumuisha ile inayotumia kuponya, inaweza kuwa njia nzuri ya kupanua mawazo kuhusu rasilimali kutoka sehemu ya 2. Aliamua kuwasiliana na wataalam saba wa mimea wanaoishi karibu na shule na kuwaalika kuja shule kuhojiana na wanafunzi katika siku iliyopangwa. Walikubali kukusanya baadhi ya mimea muhimu iliyopo katika maeneo yao ili kuwaonesha wanafunzi.

Bibi hlungwane aliwagawa wanafunzi katika makundi saba, kila kundi na mgeni wake. Alijadili na wanafunzi wake umuhimu wa kuonesha heshima kwa wageni. Kwa pamoja waliandika orodha ya maswali ya kuuliza. Alipendekeza kwamba watafiti vitu vitatu kwa kila mmea:

mmea unaitwaje;

huota wapi katika kijiji chao

Mmea wa chakula au wa dawa

Baada ya kuwashukuru na kuwaaga wageni wake, kila kundi kilitoa mlishonyuma (feedback) na Bibi Hlungwane aliandika taarifa hizo ubaoni katika sehemu tatu:

mimea ninayoiona jirani na shule

Je niyakupandwa? ( Rejea nyenzo 1: kijitabu cha taarifa za mimea)

Halafu, hujadili namna ya kutunza mimea hii kwa kuwa ni rasilimali muhimu kwa jamii. Wanaamua kuwa kujifunza kwa kutambua mimea bila kuitoa mahali ilipo ni muhimu. Pia kwamba wasiikanyage au wasiharibu mazingira inamoota 

Mwisho, Bibi Hlungwana huwataka wanafunzi katika makundi kutengeneza majumuisho ya mimea muhimu kuonesha matumizi ya kila mmea na wapi unapatikana.

Shughuli ya 1: Utafiti wa rasilimali mimea ya mahali

Jedwali litawasaidia wanafunzi kuona nini hasa wanatakiwa kufanya.

Mtake kila mwanafunzi kuchora jedwali na kuandika uchunguzi wake. Chora jedwali ubaoni ili wao wanukuu.

Jina la mmea unapatikana wapi? Tunautumia? Kwa namna gani?

Wapeleke nje katika jozi kwenye mazingira yanayoizunguka shule, kwa dakika kama 30 na watake kujaza kwa uchache misitari mitano ya jedwali. Tembea na wanafunzi na wasaidie.

Kama wanafunzi hawajui jina la mmea, wahamasishe kutoa maelezo au kuuchora kwa utambuzi baadae.

Wanaporudi darasani chora jedwali kubwa ubaoni. Zunguka darasa na jaza taarifa za wanafunzi wote kwenye jedwali hilo

Waulize wanafunzi nini wamejifunza kutokana na kipindi cha leo kuhusu mazingira asilia na aina za rasilimali ilizonazo kwa jamii.

Sehemu ya 4: Utafiti wa mabadiliko wa Mazingira