Somo la 2

Kwa kuwa mazingira asili yetu yanaweza kutupatia mahitaji yetu, unahitajika kuwashawishi wanafunzi wako kufikiri juu ya namna ya kutunza mazingira ili yaendelee kutupa tunachohitaji.

Ili wanafunzi wako waanze kufikiri kuhusu uharibifu wa mazingira unaofanyika, unaweza kuwaonyesha madhara ya uchafuzi wa mazingira. Hiki ndicho mwalimu katika uchunguzi kifani 2 alifanya kwa darasa lake. Shughuli 2 inaonesha njia nyingine-kufanya jaribio linaloonesha madhara ya uchafuzi wa maji au uhaba wa maji katika ukuaji wa mimea. Mara wanafunzi wakiona madhara yaliyotokana na uchafuzi huo, watakuwa katika hali nzuri ya kukuza mtazamo chanya juu ya utunzaji wa mazingira

Uchunguzi kifani ya 2: Kutumia ziara za mafunzo kutafiti uchafuzi

Hema Joto, mwalimu wa darasa la sita katika shule ya msingi Wema, anataka kukuza upeo wa wanafunzi juu ya madhara ya uchafuzi ya maji (Rejea Nyenzo 2: masuala ya maji kwa taarifa za msingi). Anagundua kuwa anaweza kufanya hili kwa kuwapeleka ziara ya mafunzo kwenye mto uliojaa takataka.

Mtoni, anawataka wanafunzi kutengeneza orodha ya kila kitu wanachokiona kinachafua maji. Wanafunzi walipokuwa wamefanya hilo, walikaa kwenye ukingo wa mto na Hema aliwauliza maswali ya msingi kuwahamasisha kufikiri zaidi ya kile wanachokiona. Kwa mfano aliwauliza kuwa, watu wangapi wanategemea mto huu?

Nini kingetokea kwa watu wote kama maji ya mto yangechafuliwa? Wanatumiaje maji haya?

Darasani, aliwataka kila kundi kueleza njia za kusaidia kusafisha mto na mazingira yake. Kadili anavyozunguka zunguka darasani, husikiliza na

kuwasaidia. Alishangazwa na mawazo waliyokuwa nayo wanafunzi. Mawazo hayo yalijumuisha, kuihusisha jamii na shule kuzuia uchafuzi sio kwenye mto tu bali na maeneo mengine ya kijiji. Hema alijisikia amefanikiwa lengo la kukuza upeo wa madhara ya uchafuzi wa maji na aliridhishwa na ushawishi wa mtazamo wa wanafunzi kwa jamii.

Shughuli ya 2: Jaribio la uchafuzi

Kujikumbusha au kukuza upeo wako kuhusu masuala ya maji soma Nyenzo 2. Jaribu shghuli hii mwenyewe kabla ili uwasaidie vizuri wanafunzi wako

Watake wanafunzi wako kufanya jaribio litakalochukua siku tano, ilivyoelezwa katika Nyenzo 3: Jaribio la mbegu za mahindi

Halafu watake kila mwanafunzi kuandika utabiri wake juu ya kitakachotokea kwa kila mbegu kwa siku tano.

Watake kuangalia maendeleo ya mbegu zote tatu kila siku

Wanafunzi watengeneze dondoo za uchunguzi wao wa kila siku. Unaweza kuhusika kwa kutengeneza dondoo zako mwenyewe.

Siku ya tano, fanya majadiliano ya kina pamoja na wanafunzi kuhusu kama utabiri wao umetokea au haukutopkea. Nini kimetokea kwa kila mbegu?Jadili matokeo ya jaribio kwa kuzingatia uchafuzi. Mnaweza kufikiri jaribio jingine juu ya uchafuzi wa mazingira