Somo la 3

Wanafunzi wengi wamevutiwa na kile kinachotokea katika mazingira yao na matumizi ya rasilimali kama magazeti au redio vinaweza saidia kuimarisha kipindi chako.

Lengo la shughuli muhimu ni kuhamasisha wanafunzi kufikiri jinsi mabadiliko ya hali ya hewa duniani yanavyoweza kuathiri mazingira ya mahali fulani, na kuwapa wazo la kuongezeka kwa joto kama maelezo yanayoweza kusababisha mabadiliko ya hali ya hewa.katika uchunguzi kifani 3, mwalimu alitumia taarifa za mahali kama sehemu ya kuanzia kufundisha juu ya mzunguko wa maji.

Mara wanafunzi wakiweza kuona uhusiano baina ya matukio unaweza kuanza kupanua ujuzi wao wa kufikiri kwa kina. Ujuzi huo utawasaidia kujenga hisia juu ya kila badiliko katika dunia wanamoishi

Uchunguzi kifani ya 3: Matumizi ya magazeti katika kufundisha mzunguko wa maji

Kumekuwa na mijadala mingi kuhusu maji katika magazeti wiki lililopita. Matumizi ya maji yamezuiwa. Maji yaingiayo bwawa la Pangani ni kidogo. Kulikuwa na uzalishaji mdogo kaskazini mwa nchi

Muhgare aliona uwezekano wa kujadili masuala ya upatikanaji wa maji na wanafunzi wake. Aliandika swali hili ubaoni. ‘mvua yote huenda wapi ardhi inapokauka? Na halafu aliwataka kila kundi la wanafunzi kuongelea hili kwa dakika kumi. Wakati huo alizungukia makundi na kuhamasisha kila mmoja kutoa mawazo yake

Halfu Muhgare alikusanya wanafunzi kumzunguka na aliwataka kubadilishana mawazo. Wanafunzi kwa pamoja walielewa kuhusu mzunguko wqa maji ( Rejea Nyenzo 4: Mzunguko wa maji)

Muhgare alimaliza kwa kuchora mchoro unaoonyesha mzunguko wa maji ubaoni na kuwataka wanafunzi kunakili mchoro huo.

Shughuli muhimu: Ongezeko la joto

Soma Nyenzo 5: makala yanayohusu ongezeko la joto kabla ya kipindi

Gawanya darasa katika makundi madogo na halafu wasomee makala au wape kila kundi nakala ya kusoma pamoja

Waelezee wanafunzi kuhusu mfumo wa barafu ya Kilimanjaro katika miaka kumi iliyopita( Rejea Nyenzo 6: Barafu ya Kilimanjaro)

Waamuru kila kundi kutoa bango au mchezo mfupi kujibu maswali yafuatayo

Nini kinasababisha ongezeko la joto?

Ni madhara gani yanaweza kusababishwa na ongezeko la joto? Nini tunaweza kufanya kupunguza ongezeko la joto? Utawaulizaje wanafunzi kutathmini kazi yao?

Unaweza kushirikishana kazi ya wanafunzi juu ya ongezeko la joto pamoja na wanafunzi wengine.

Nyenzo-rejea ya 1: Kijitabu cha mimea