Nyenzo-rejea 2: Masuala ya maji
Nyenzo za mwalimu kwa kuandaa au kubadili kwa matumizi ya wanafunzi
Uchafuzi wa maji
Uchafuzi husababiswa na:
- Takataka na mbolea za chumvuchumvi
- Matope na mchanga (mkusanyiko wa mawe ambao huwa katika matabaka)
- Malighafi zitokanazo na viumbe hai kama majani na nyasi zilizo katwa
Matumizi ya maji
Matumizi ya maji duniani yameongezeka mara sita zaidi kati ya mwaka
1900 na 1995 zaidi ya mara mbili ya kiwango cha ongezeko la watu-na huendelea kukua kadri kilimo viwanda na matumizi ya nyumbani yaongezekavyo. Kilimo hutumia takribani asilimia 70 ya matumizi yote ya maji duniani. Maji yatahitajika zaidi kadri watu watakavyoongezeka- inakadiriwa kuwa watu wataongezeka kutoka bilioni 6 sasa hadi bilioni8.9 ifikapo mwaka 2050
Tunaohitaji maji sio sisi tu bali kila kiumbe kinachoishi katika dunia hii pamoja nasi-na mfumi-kolojia ambapo viumbe hutegemeana
Ugonjwa
Zaidi ya watu milioni tano hufa kutokana magonjwa yatokanayo na maji kila mwaka –mara kumi ya idadi ya watu wanaokufa kutokana na vita.
Mabadiliko ya hali ya hewa
Mabadiliko ya hali ya hewa yatakuwa na athari. Baadhi ya maeneo yanaweza kufaidika na ongezeko la mvua, lakini maeneo mengine huathirika kutokana na ongezeko hilo la mvua.Tunatakiwa kufikiri tena
kwa kiwango gani tunahitaji maji kama tunajifunza namna ya kushirikiana maji. Wakati mabwawa na miradi mingine mikubwa ikiwa na umuhimu mkubwa kwa jamii duniani kuna ongezeko utambuzi wa thamani ya kutumia maji tuliyo nayo vizuri kuliko kuvuna maji bila mpangilio. Mamilioni ya watu duniani hutegemea maji ili waishi, na kukosekana kwake hupelekea kifo.
Mgawanyo wa maji duniani
Nyenzo-rejea ya 1: Kijitabu cha mimea