Nyenzo-rejea: 5: Makala inayohusu kuongezeka kwa joto

Taarifa za musingi/ ujuzi wa mada kwa mwalimu

Makala

Ongezeko la joto linasababisha mabadiliko ya hali ya hewa duniani, au vipindi virefu vya hali ya hewa, ambavyo hutofautiana kutoka eneo moja hadi jingine. Kadili dunia inavyozunguka,joto jipya huzunguka pamoja na dunia, ikichukua mvuke kutoka baharini, huongezeka hapa kutua mahali. Inabadilisha uwiano wa hali ya hewa ambayo viumbe hai hutegemea.

Tutafanya nini ili kupunguza ongezeko la joto? Namna gani tutabadilika ili kuendana na mabadiliko ambayo tayari tunayo? Wakati tukipambana na hili, sura ya dunia tunayoifahamu –pwani, misitu, mashamba na barafu iliyofunika milima vinatoweka.

Athari za gesi joto

Athari za gesi joto ni ongezeko la joto ambalo hutokea wakati gesi fulani angani zinapofyonza joto. Gesi hizi huruhusu mwanga lakini kama ukuta wa kioo wa nyumba za kuzalishia mimea hutunza joto lisipotee.

Kwanza,mionzi ya jua hutua kwenye uso wa dunia ambapo hufyonzwa na halafu mionzi hiyo hurudi tena angani kama joto. Angani, Gesi joto hufyonza baadhi ya joto na joto jingine hupotea hewani.Kadili gesijoto zinavyoongezeka angani ndivyo joto hufyonzwa zaidi.

Wanasayansi walijua juu ya athari za gesijoto tangu 1824,na wamekokotoa kuwa dunia ingekuwa baridi sana kama kusingekuwa na anga. Athari za gesijoto ndizo zinazofanya hali ya hewa ya duniani iweze kuishika.Bila hiyo,sura ya dunia ingekuwa na wastani wa kiwango cha 60 oF cha baridi. Binadamu huweza kuongeza kiasi cha gesi joto kwa kutengeneza gesi za kaboni dioksaidi (co2)

Kiwango cha gesi joto kimekuwa kikiongezeka na kupungua katika historia ya dunia, lakini kimekuwa hakibadiliki kwa miaka elfu iliyopita. Wastani wa kiwango cha joto duniani kimekuwa cha kawaida tangu muda mrefu hadi hivi karibuni. Kupitia kuchoma mabaki ya mafuta na utoaji

gesi joto, binadamu wanaongeza athari za gesi joto na ongezeko la joto duniani.

Kwa kawaida wanasayansi hutumia neno “mabadiliko ya hali ya hewa” badala ya ongezeko la joto duniani.Hii ni kwa sababu kadili wastani wa joto unavyoongezeka duniani upepo na mikondo ya bahari inaondoa joto kwa njia ambazo zinaweza kusababisha baridi baadhi ya maeneo, joto na kubadili kiwango cha mvua na kiasi cha barafu. Matokeo yake, hali ya hewa hubadilika tofauti katika maeneo tofauti.

Je mabadiliko ya joto sio ya asili?

Wastani wa joto duniani na kiwango cha kaboni dioksaidi (moja ya gesi joto) kimepungua kwenye mzunguko kwa mamia ya maelfu ya miaka kulingana na sehemu ilipo dunia na jua vinavyotofautiana. Matokeo yake, theruji inakuja na kupotea.

Hata hivyo, kwa miaka mingi sasa, uzalishaji wa gesi joto angani umewianishwa na gesi joto zilizozinafyonzwa kiasili .Matokeo yake kiwango cha gesi joto na joto vimekuwa sawa(havibadiliki).Usawa huu umeruhusu jamii ya watu kuendelea kuwepo katika hali ya hewa isiyobadilika.

Mara chache,sababu nyingine huchangia kuongezeka au kupungua kwa joto. Kwa mfano milipuko ya volkano hutoa chembechembe ambazo huifanya sura ya dunia kuwa ya baridi kwa muda. Lakini hizi zina madhara yasiokwisha katika miaka machache.

kwa sasa,binadamu wameongeza kiwango cha karbon dioksaidi angani kwa zaidi ya theruthi tangu mapinduzi ya viwanda.Mabadiliko haya makubwa yana historia ya miaka mingi,lakini kwasasa yanatokea zaidi ya mwendo wa miongo mingi.

Kwanini hili ni tatizo? 

Ongezeko la haraka la gesi joto ni tatizo kwa sababu linabadilisha hali ya hewa kwa haraka kuliko baadhi ya viumbe hai vinavyoweza kubadilika. Pia hali ya hewa mpya na isiyotabirika hutoa changamoto ya pekee kwa maisha.

Kihistoria, hali ya hewa duniani mara nyingi imebadilika, joto limepungua na kuongezeka kama hili tunaloliona leo na baridi kali iliyofunika sehemu kubwa ya Amerika na Ulaya. Utofauti kati ya kiwangi cha joto duniani cha leo na cha wakati wa barafu ni 5 centigradi na hutokea taratibu,kwa miaka mingi kwa sasa, kwa kiwango cha gesi joto kupanda, sehemu zilizobaki na barafu duniani (kama Greenland na Antaktika) nako barafu

imeanza kuyeyuka pia. Maji ya ziada yanaweza kuongeza kina cha bahari.

Hali ya hewa inaweza kubadilika kwa njia isiyotegemewa. Mbali na Kuongezeka kwa kina cha bahari , hali ya hewa inaweza kuwa baridi au joto kuzidi kiwango. Hii ina maana mvua kubwa zaidi za mawe, mvua nyingi zikifuatiwa na vipindi virefu vya ukame(changamoto kwa uzalishaji wa mazao), mabadiliko katika kiwango ambacho mimea na wanyama wanaweza kuishi,na upungufu wa maji ambayo kihistoria yametoka na barafu.

Wanasayansi wameshaona baadhi ya haya mabadiliko yanatokea haraka zaidi kuliko hata ilivyotegemewa.Miaka 11 kati 12 ya joto jingi tangu kumbukumbu zianze kupatikana ilikuwa kati ya mwaka 1995 na 2006.

Makala ya 2 inangalia madhara ya kuongezeka kwa joto Afrika. Bara la Afrika ni tajiri kwa mfumi-kolojia mbalimbali,unaonzia theruji na barafu ya mlima Kilimanjaro misitu ya tropiki hadi jangwa la sahara.Hata kama lina matumizi madogo ya nguvu kuliko mabara mengine duniani, Afrika linaweza kuwa bara linalodhurika kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa kuliko mengine mengine kwa sababu ya umasikini mkubwa unaozikumba nchi nyingi za Kiafrika na kukosa uwezo wa kubadilika. Dalili za

mabadiliko ya hali ya hewa Afrika zimeshaonekana: mlipuko wa magonjwa na kuyeyuka kwa barafu milimani,kuongezeka kwa joto jangwani na maeneo mengine,kuongezeka kwa kina cha bahari na kuchubuka kwa marijani kandokando ya bahari. Yafuatayo yanaonesha baadhi ya matukio yanayoelekeana

Cairo, Misri – Agosti yenye jot jingi zaidi katika kumbukumbu

1998. Joto lilifikia41 °C (105.8 °F) Agosti 6, 1998.

Afrika ya kusini- muongo wa joto jingi na ukame katika kumbukumbu , 1985–1995. Wastani wa joto uliongezeka kwa kiasi cha

0.56 centigradi ukilinganisha na kalne iliyopita.

Senegali-ongezeko la kina cha bahari. ongezeko la kina cha bahari inasababisha kupotea kwa ardhi iliyopo ufukweni Rufisque katika pwani kusini mwa senegali.

Kenya –katika mlima Kenya kiwango kikubwa cha barafu kinapotea. Asilimia 92 ya barafu ya lewis imeyeyuka miaka mia moja iliyopita. Bahari- kupata joto kwa maji. Bahari imekuwa ikipata joto linalofikia nyuzi 0.06 centigradi kutoka usawa wa bahari hadi kina cha

3,000m kwa miaka 35-45 iliyopita . zaidi ya nusu ya ongezeko la joto imetokea juu zaidi ya m 300. Kupata joto kwa maji kunatokea katika mabonde yote ya bahari na sehemu zenye kina kirefu kulikoilivyofikiriwa kabla.

Milima ya Ruwenzori-Uganda –Kutoweka kwa barafu.Tangu miaka ya

1990 eneo lenye barafu limepungua kwa asilimia 75. katika bara la Afrika joto limeongezeka kwa kiwango cha 0.5 centigradi kwa karne iliyopita, na miaka mitano ya joto katika Afrika imetokea tangu mwaka 1988.

Kenya-Mlipuko wa ugonjwa wa malaria, majira ya joto, 1997

Mamia ya watu walikufa kutokana na malaria kwenye miinuko nchini

Kenya ambako watu hawakuwa na uelewa juu ya malaria.

Tanzania – Malaria huongezeka milimani..Kiwango cha juu cha joto la mwaka katika milima ya Usambara kimehusianishwa na kuenea kwa malaria.

Bahari ya hindi, Ghuba ya Persian, visiwa vya Shelisheli – Kuchubuka kwa mwamba wa marijani. Inajumuisha Shelisheli; Kenya; Somalia;Madagaska ;Maldives;Indonesia;Sri-lanka; ghuba ya Tailend Visiwa vya Andamani;Malesia;Omani;India na Kambodia.

Kenya-ukame mkali katika miaka 60, 2001.Zaidi ya watu millioni nne waliathirika na upungufu mkubwa wa mavuno kudhoofika kwa mifugo na hali mbaya ya usafi.

Ziwa Chadi-kupotea kwa ziwa..Sura ya eneo la ziwa imepungua

kutoka mita za mraba 9,650 (25,000 Kilometa za mraba) ndani ya mwaka

1963 hadi mita za mraba 521 (1,350 kilometa za mraba) kwa sasa. Mafunzo ya sasa yanaashiria upungufu mkubwa wa maji unatokana na muunganiko wa upungufu wa mvua na ongezeko la mahitaji ya maji kwa kilimo cha kumwagilia na mahitaji mengine ya binadamu.

Afrika kusini –Uchomaji wa fukwe. Januari 2000

Moja ya miezi ya kumi na mbili kame iliyo katika kumbukumbu, na joto zaidi ya sentigredi 40 ilichoma moto pwani ya magharibi mwa mkoa wa Cape. Kiasi kikubwa cha moto uliochomwa kilichochewa na uwepo wa aina mbalimbali za mimea vamizi, ambayo baadhi hutoa asilimia 300 zaidi ya joto ikichomwa ikilinganishwa na mimea asili.

Imenukuliwa kutoka: Climate Hot Map, Website

Nyenzo-rejea 4: Mzunguko wa maji

Nyenzo 6: Barafu ya mlima Kilimanjaro