Nyenzo 6: Barafu ya mlima Kilimanjaro

Nyenzo za mwalimu kwa kuandaa au kubadili kwa matumizi ya wanafunzi

Kama baba yake kabla yake, Munyai alifanya kazi kama kiongozi katika mlima Kilimanjaro. Kila mwaka huongoza makundi mawili ya watalii mpaka kileleni. Amekuwa akifanya kazi hii kwa miaka mitano na hakumbuki ni mara ngapi amepanda mlima huo. Leo yuko kileleni, akizungumza na baadhi ya watalii wa Kiswisi kuhusu kupanda mlima na wameshafika kileleni. Mmoja anatoa maelezo ya kushangazwa na ukweli kuwa hakuna barafu juu ya mlima kwa sasa. Mnyai anagundua kuwa miaka miwili tu iliyopita barafu ya mlima Kilimanjaro imepotea na anashangaa kwanini. Anaporudi nyummbani anamwuliza baba yake kama anakumbuka kama kuna wakati kulikuwa hakuna barafu juu ya mlima. Jibu la baba yake ni la wazi-kuwa kulikuwa na barafu muda wote!

Picha za barafu na theruji juu ya Mlima Kilimanjaro

Mlima Kilimanjaro umekuwa ukijulikana ‘Mlima unaong’ara’. Baadhi ya wanasayansi wanasema kilele cha Mlima Kilimanjaro kinaweza kising’are tena. Kwa mujibu wa profesa Lonnie Thompson wa Chuo Kikuu Ohio, theruji ya Mlima Kilimanjaro inaweza kupotea mwaka 2020. Katika makala yake ya tarehe 18 Oktoba jarida la sayansi, Thompson na waandishi wenzake waligundua kuwa theruji kileleni ambayo iliyokuwepo zaidi ya miaka 11000 iliyopita imepungua kwa asilimia 82% kwa karne iliyopita. Waandishi wametammbua kuwa kupungua kwa kasi kwa theruji kwa siku za karibuni ni kwa kushangaza ukizingatia uwezo wake wa kustahmili mabadiliko mengi ya hali ya hewa., ikijumuisha ukame mkubwa wa miaka 300 ambao uliathiri maisha ya watu walioishi kuzunguka eneo hilo yapata miaka 4000 iliyopita.

Picha zinaonesha mitazamo miwili kuhusu mlima Kilimanjaro, tarehe 17

Februari 1993(juu), na tarehe 21 Februari 2000 (chini). Picha hizi zilipigwa na kipimo cha satilaiti 5 na 7, moja-moja. Madhari yanaonesha uoto mkubwa (wa kijani) kuzunguka mlima, wakati uoto kwa wastani upo mbalimbali hadi urefu wa mita 5,895. rangi ya kahawia sehemu ya juu ya Mlima inaonesha mawe na ardhi tupu, kuonesha mifumo ya maji inayokatizana yatokanayo na mvua na kuyeyuka kwa barafu katika mlima Kilimanjaro.

Chanzo: NASA Earth Observatory, Website

Nyenzo-rejea: 5: Makala inayohusu kuongezeka kwa joto

Sehemu ya 5: Kuwapeleleza watu wengine na maeneo