Sehemu ya 5: Kuwapeleleza watu wengine na maeneo

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kuwasaidia wanafunzi watambue uhusiano wa kufanana kwa watu tofauti na mahali tofauti?

Maneno muhimu: Utafiti, maeneo, mazingira

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Unatambua tofauti na kufanana katika muktadha/mazingira mbalimbali ya Africa;
  • Utakuwa umetumia mbinu za kimawasiliano zinazohusu kufananisha jamii na matendo katika mazingira/ muktadha wowote;
  • Kupanga kazi ya utafiti darasani kwa kutumia nyenzo mbalimbali.

Utangulizi

Unapofundisha masomo ya kijamii, muda wote unakutana na maswali ya utofauti na ukawaida/ufanano.

Sehemu hii imeangalia namna unavyoweza kuwasaidia wanafunzi wako kulinganisha maisha na matendo ya kiuchumi katika mazingira mbalimbali. Hii itasaidia kujenga uwezo muhimu wa kifikra katika taaluma ya maarifa ya jamii kwa wanafunzi wako na wewe mwenyewe..

Nyenzo 6: Barafu ya mlima Kilimanjaro