Somo la 1

Katika shule ya msingi wanafunzi wakubwa wanaweza kufanya kazi kwa wazo kuwa vitu katika makundi mawili tofauti vinaweza kuwa na sifa nyingi zinazovifanya kuwa sawa. Ni sehemu ya majukumu yako kuwasaidia wanafunzi wa umri mdogo kulijua hili.

Katika sehemu hii, unahimizwa kuwajengea wanafunzi wako wazo hili katika mahusiano kati ya ukawaida na utofauti walionao wanadamu. Uchunguzi kifani 1 na shughuli 1 vinapendekeza njia za kutumia makundi ya majadiliano kutambua aina tofauti za maisha ya watu katika maeneo mbalimbali, lakini pia kuwakumbusha wanafunzi kuwa watu wote kila mahali wanafanana kwa utu wao.

Uchunguzi kifani ya 1: Kutambua tofauti katika makazi

Bi. Maryogo anafundisha Jiografia katika shule ya kijijini nchini Tanzania. Wakazi wa kijiji hiki ni maskini sana. Bi Maryogo anataka kuwasaidia wanafunzi wake kujua tofauti zilizopo katika jamii, hivyo anawapa kazi zinazowachochea kutafakari kwa undani/kudadisi ili wagundue wenyewe ukweli juu ya dunia wanayoishi.

Leo, amepanga kwa umakini anachoweza kutarajia wanafunzi wake wa miaka 11 wafanye na ameandaa mlolongo wa picha zinazoakisi maisha katika jamii tofauti. (Angalia nyenzo rejea 1: kuishi katika jamii tofauti).

Katika majadiliano darasani, Bi Maryogo anatoa maswali yafutayo: Vitu/mambo gani ya maeneo haya yanafana?

Jinsi gani watu wanaoishi sehemu hizi wanafanana?

Kuna tofauti gani?

Kwa nini kuna tofauti hizi?

Wanafunzi wanapopendekeza majibu ya maswali haya, anawahimiza kupanua mawazo yao ili wafikiri kwa undani zaidi. Anaibua hisia zao juu ya wanavyohisi kuishi kijijini kwao . (Pia angalia nyenzo rejea muhimu: kutumia maswali kuhamasisha kufikiri)

Shughuli ya 1: Tuko tofauti, tuko sawa.

Gawanya darasa lako katika makundi ya wanafunzi wanne au zaidi (kama itawezekena kuzalisha nakala chache za nyenzo rejea 1 : basi makundi yako yatakuwa makubwa).

Lipe kila kundi matukio kuanzia nyenzo rejea 1 -kusoma shule, kuogelea au kuhemea –ili wazifanye kazi. Kila kundi liandae orodha ya mfano wa kila hali, na tofauti zilizopo. Tumia ushahidi uliopo kwenye picha tu.

Waambie kila kundi waandike sentensi zinazolinganisha hali hizo za kila mfano.

A: Sokoni bidhaa za chakula zimepangwa kwenye sinia la duara B: Dukani,watu husukuma bidhaa kwenye vigani vya kubebea Wanaweza kuzionyesha sentensi hizi na picha darasani ili waweze

kuona/angalia nini makundi tofauti yanasema juu ya picha.

Ukiangalia kwenye maonyesho yao utagundua namna walivyoelewa mada. Unaweza kutumia hili kupanga hatua inayofuata katika kujifunza kwao.

Kama una wanafunzi wa umri mdogo, unaweza kufanya kama shuguli ya darasa, kwa kutumia picha mbili zinazokinzana na kuwauliza wanafunzi ili kuwasaidia kuelekeza ugunduzu wao.

Sehemu ya 5: Kuwapeleleza watu wengine na maeneo