Somo la 2

Kuwapa nafasi wanafunzi wako wapate habari juu ya hali tofauti kutawasaidia kuelewa tofauti kati ya jamii. Uchunguzi kifani 2 na shughuli 2 vinaonyesha njia tofauti za kuwapanga wanafunzi na kutumia maswali kuruhusu fikra juu ya ufanano na tofauti.

Uchunguzi kifani ya 2: Kutumia maswali kulinganisha maeneo mbali mbali

Bi. Maryogo ameandaa somo juu ya kugundua tofauti na ufanano kati ya maeneo tofauti ya kienyeji. Ameandaa karatasi yenye maelekezo kati ya maeneo mawili tofauti ( Angalia nyenzo rejea 2: Kulinganisha Magubike na Gairo). Mwanzoni mwa somo, anatoa karatasi na anawaambia wanafunzi wazifanyie kazi kwenye makundi yao.

Anaandika maswali yafutayo ubaoni;

Yapi yanafanana na yapi ni tofauti kati ya haya mazingira mawili (Magubike na Gairo)?

Je, Kuna viwango vya kufanana vya maisha kwa haya mazingira mawili? Wakati makundi haya yanafanya kazi Bi Maryogo anazunguka akisikiliza

mazungumzo yao na kuwaunga mkono kwa kutafakari kwa kina.

Anawauliza maswali kulingana na yale wanayosema wanafunzi ili awasaidie kufikiri, na anazingatia mawazo yao na mitazamo zao.

Bi Maryogo anahakikisha kila wakati kwamba amejipanga vizuri ili aweze kuangalia zaidi maendeleo ya uelewa wa wanafunzi wake.

Shughuli ya 2: Kulinganisha mazingira mawili tofauti:

Shughuli hii inawapa fursa wanafunzi kutazama mazingira tofauti ya kijamii

Unaweza ktumia nyenzo rejea 2 au kutengenza mazingira yako tofauti (labda kwa kutumia picha za magazeti) Lipe kila kundi picha mbili tofauti: ( nyenzo rejea ya muhimu 2: kutumia kazi za makundi darasani kwako). Waambie waainishe sifa za kila mazingira kwa kuzingatia mambo kama sifa za kimazingira, shughuli za kiuchumi na kazi ambazo watu hufanya. Wanaweza kutofautisha picha na mahali wanapoishi. Waambie waandike sifa na mawazo muhimu kuhusu kipi ni tofauti na vipi vinafanana.

Weka makundi mawili pamoja na wambie kila kundi kushirikishana mawazo yao.

Liambie kila kundi kueleza walichotafiti darasani.