Somo la 3

Baada ya kutambua tofauti na kufanana kati ya eneo la kijiografia na darasa lako, hatua inayofuata ni kutumia mawazo haya kwa kuwahusisha wanafunzi wako kutafakari njia za kuboresha mazingira yao. Uchunguzi kifani 3 unaonyesha namna mwalimu alivyotengeneza bustani ya shule kama sehemu ya masomo yake ya Sayansi na Maarifa ya Jamii; Shughuli muhimu huwasaidia wanafunzi kuchunguza jinsi mazingira yao yanavyoweza kuboreshwa.

Uchunguzi kifani ya 3: Kutengeneza mazingira ya shule

Bi Mgude anafundisha somo la Maarifa ya Jamii kwa wanafunzi wake wa darasa la 4 na la 5 kusini magharibi mwa Tanzania. Amekuwa akilinganisha mazingira ya sehemu mbalimbali akichunguza jinsi yanavyofana pia tofauti zake. Anataka wanafunzi wake watumie habari hizi kutafakari namna wanvyoweza kuboresha mazingira yao shuleni kwa njia endelevu (angalia Nyenzo rejea 3: Elimu kwa maendeleo endelevu).

Baada ya majadiliano ya kutosha, wanafunzi wake waliamua kua wangependelea kuandaa maeneo ya kukaa kwenye bustani na pia kupaka rangi kwenye uwanja wa michezo au kutengeneza michezo ya kucheza wakati wa mapumziko. Aliwaruhusu wanafunzi kujadii kwenye makundi yao. Walihitaji kufikiri juu ya:

Pa kuweka viti;

Watavitengeneza kutokana na nini; Kupata ruhusa toka kwa mwalimu mkuu;

Kuwahusisha wazazi na wajumbe wengine katika jamii; Michezo gani wanayopenda;

Wakiwa pamoja awalipanga ratiba ya kazi iliyobandikwa ukutani. Mwalimu

mkuu aliomba kuhudhuria na kusikiliza mawazo yao.

Shughuli muhimu: Kuboresha mazingira.

Waulize wanafunzi wako wanapenda nini kwenye jamii yao na mazingira yao, kisha viorodheshe ubaoni.

Halafu waambie watafute njia za kuboresha mazingira ya shule yao

Waulize maswali haya mawili ili kuwafanya waanze kuongea Utafanyaje mazingira ya shule yavutie wakati wa michezo? Utamhamasishaje kila mtu ili ajivunie na kulinda shule?

Kila kundi litakapokuwa linatoa mawazo, orodhesha mawili ambayo ni maarufu ubaoni. 

Wakati ambao kila kundi limetoa marejesho, pitia kila pendekezo kwa kutoa ufupisho wa kila suala.

Waambie wanafunzi wako (mmoja mmoja au kama kundi) kutengeneza mpango wa chaguo lao la namna ya kuborehsa mazingira, na kuubandika ukutani.

Nyenzo-rejea ya 1: Kuishi kwenye jamii tofauti